ad

ad

ISIPOSHIRIKI UEFA, ZLATAN ANAONDOKA ZAKE MAN UNITED


Mshambuliaji mkongwe Zlatan Ibrahimovic anaweza kuondoka Manchester United ikiwa timu hiyo itashindwa kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hiyo inamaanisha kuwa lazima timu hiyo iwemo katika timu nne za juu katika Premier League au kushinda taji la Europa League ili kumshawishi mchezaji huyo abaki.

Taarifa kutoka ndani ya United zinaeleza kuwa Ibrahimovic, 35, bado hajafikia muafaka wa mkataba mpya kwa kuwa anasubiri kuona muelekeo wa timu yake.

Tayari kuna ofa amepata kutoka Marekani na China ambapo kote wamemtengea dau nono ikiwa atataka kuondoka klabuni hapo.

Ikiwa United itatwaa ubingwa huo wa Europa League itafuzu kuingia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa moja kwa moja.

No comments

Powered by Blogger.