SI KITU BILA PENZI LAKO -04
Maisha mapya yakaanza katika Kijiji cha Itilima. Kila siku Bi Anna
alionekana kuwa na majonzi, furaha kwake haikuwa sehemu ya maisha yake
kabisa. Kichwani mwake, taswira ya marehemu mumewe bado ilimsumbua, kila
siku ndoto juu ya mumewe zilikuwa zikimjia.
Hakujua katika kipindi hicho mtoto wake Patrick alikuwa hai au vipi ingawa moyoni mwake alikuwa na uhakika asilimia mia moja kuwa Patrick alikuwa ameuawa. Kila siku alimuomba Mungu juu ya familia yake, kama Patrick aliuawa basi Mungu amlinde mahali pema peponi lakini kama alikuwa hai basi aendelee kumlinda kila siku.
Miezi miwili ilkapita, Bi Anna alikuwa akifanya kazi kwa juhudi zote katika shamba la Mzee Ubuge kiasi kwamba kila mtu alishangazwa naye. Wanawake wengi wa Kijiji cha Itilima walikuwa wakielekea shambani kulima huku wanaume wakibaki nyumbani wakipiga soga.
Bi Anna alikasirika hali iliyomfanya kuanzisha kikundi kidogo cha wanawake kumi ambacho kilihusika na haki za wanawake kijijini hapo. Kila siku alikuwa akiwaita wanawake hao na kuongea nao. Sifa za kikundi kile zikaanza kusambazwa sehemu mbalimbali. Kila mwanamke akawa na hamu ya kutaka kujiunga nao.
Mpaka mwezi mmoja unakatika baada ya kuanzisha kikundi kile, wanawake zaidi ya hamsini walikuwa wamejiunga nao. Walikuwa wakikutana na kuongelea mambo mbalimbali kuhusu maendeleao kijijini hapo. Hawakutaka kabisa kufanyishwa kazi kama punda huku waume zao wakiwa nyumbani wakipiga soga na kunywa kahawa.
Kila siku kelele zao zilikuwa ni kuwataka waume zao wawasaidie kazi mbalimbali kama kulima na kazi nyingine badala ya kubaki nyumbani tu. ujumbe mbalimbali kutoka katika kikundi kile zilipuuzwa na wanaume wote lakini kadiri siku zilivyokwenda mbele ndivyo wanachama wakazidi kuongezeka.
Wanachama waliongezeka zaidi na zaidi huku Bi Anna akiwa mhamasishaji na kupewa uongozi wa kuwa mwenyekiti. Wanawake wengi kutoka katika vijiji mbalimbali wakaanza kujiunga na kikundi hicho kilichopewa jina la WAMASHI iliyomaanisha WANAWAKE WA MAENDELEO SHINYANGA.
“Tunahitaji mabadiliko katika jamii zetu....tunahitaji kusaidiwa katika kila kazi ambayo tunaifanya na si kila kazi kufanya sisi huku ninyi wanaume mkipiga soga tu,” Bi Anna alisema katika mkutano wa wazi ambao ulifanyika katika Kijiji cha Itilima.
Wanaume walibaki wakiangaliana kwa aibu. Maneno aliyoyaongea Bi Anna yalimgusa kila mtu. Kila wakati vigelegele vilisikika kutoka kwa wanawake waliokusanyika mahali hapo.
“Mabadilikoooooo...........” Bi Anna alisema kwa sauti kubwa iliyosikika vizuri katika uwanja ule.
“Yanawezekanaaaaaaa.....” wanawake wote waliitikia kwa sauti kubwa.
*****
Mzee Carlos alikasirika mno. Alikaa kitini nje huku akiipigapiga chini fimbo aliyoishika. Moyo wake ulikuwa na hasira kali, kitendo alichokifanya Victoria cha kuondoka na Patrick kuelekea porini kilimkasirisha kupita kiasi.
Kila wakati aliiangalia saa yake iliyoonyesha kuwa tayari ilikuwa saa mbili na dakika tano usiku. Muda wote aliangalia kule kichakani ambako Victoria na Patrick walikuwa wameelekea, alionekana kukasirika mno.
Ilipotimia saa tatu kasoro, Samuel, Richard pamoja na Victoria wakaanza kuingia kijijini hapo. Mzee Carlos akasimama na kuanza kuwasogelea huku akionekana kukasirika. Muda wote Victoria alikuwa akilia. Mzee Carlos akamshika Victoria mkono na kumsogezea kwake.
“Mwenzake yuko wapi?” Mzee Carlos aliwauliza huku akionekana kuwa na hasira.
“Alikimbia. Hatujui alikimbilia wapi.”
“Niambie.....mmefanya?” Mzee Carlos aliuliza huku akionekana kukasirika. Victoria hakujibu kitu chochote kile, alibaki akilia tu.
“Niambie...mmefanya kitu chochote?” Mzee Carlos alirudia swali lake kwa hasira zaidi.
“Ndi....” Victoria alijibu akini hata kabla hajamalizia sentensi yake, akashtuka kibao kizito kikishushwa shavuni mwake.
Victoria akaanguka kama mzigo, kilio kiliendelea kusikika kwa sauti kubwa ambayo iliwakusanya watu kutoka sehemu nyingine na kuzunguka katika eneo la nyumba ile.
Bado Mzee Carlos alionekana kuwa na hasira mno, alibaki akimwangalia Victoria huku akiuma meno yake kwa hasira. Akamfuata pale chini alipokuwa amekaa na kumnyanyua. Akampiga kibao kingine cha nguvu, Victoria akaanza kuyumba, tayari akaona kulikuwa na hatari mahali hapo.
“Mwachie mwanangu,” Bi Huruma alimwambia mumewe aliyebadilika na kuwa na hasira kali kupita kawaida.
Kitendo cha mzee Carlos kumwachia Victoria kilionekana kuwa kama kosa, kwani hapohapo msichana huyo akaanza kukimbia kuelekea porini huku akilia.
Kila mtu akamshangaa Mzee Carlos, hawakujua ni kitu gani kilitokea mahali hapo. Kila mtu akamuonea huruma Victoria ambaye alikimbilia katika pori lililokuwa limezunguka kijiji hicho
Bi Huruma akawa na wasiwasi, moyoni mwake alimpenda sana binti yake, Victoria ambaye alikuwa mtoto wa mwisho na mtoto pekee wa kike. Kuondoka kwake kulimkasirisha, hakufurahishwa na hali aliyokuwa nayo mumewe.
“Mwacheni aende...atarudi tu. Mtoto mpumbavu sana yule,” alisema Mzee Carlos kwa hasira.
Sekunde ziliendelea kukatika, dakika zikaendelea kusonga mbele. Saa zilisogea zaidi lakini Victoria hakurudi mahali hapo. Kila mtu akaanza kuingiwa na wasiwasi kwamba Victoria alikuwa ameondoka moja kwa moja.
Waliendelea kuvuta subira kwa kudhani kwamba angerudi. Muda uliyoyoma lakini bado hali ilikuwa ileile, Victoria hakurudi nyumbani. Bi Huruma hakutulia, kila wakati alikuwa akiangalia porini kuona kama Victoria angerudi au la.
“Mungu wangu! Saa nane!” alisema Bi Huruma kwa mshutuko kwani mpaka muda huo bado binti yake hakuwa amerudi nyumbani.
Hakukuwa na dalili zozote za Victoria kurudi, saa zilikwenda mbele lakini wala hakukuwa na mabadiliko yoyote yale. Bi Huruma hakupata usingizi, muda wote macho yake yalikuwa wazi yakimsubiri Victoria ambaye mpaka inafika saa kumi na mbili asubuhi, hakuwa amerudi nyumbani hali iliyozua hofu kubwa kwa kila mmoja.
*****
Bado shughuli za uchimbaji wa almasi zilikuwa zikiendelea katika Mgodi wa Mwadui. Vijana waliokuwa wakifanya kazi ya uchimbaji madini katika mgodi huo walifanya kazi kwa juhudi zote kwani waliamini kama wangetoka mahali hapo, basi mafanikio yalikuwa pamoja nao.
Kila siku vijana wengi waliongezeka mgodini hapo na kuajiriwa na makampuni mbalimbali yaliyozidi kuongezeka. Kila mtu alihitaji kupata fedha na ndiyo kitu kilichowafanya kufanya kazi kwa nguvu zote.
Mji wa Mwadui ukaanza kubadilika, huduma zote za kijamii kama maji na umeme vikaletwa mahali hapo. Shule zikajengwa kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi mchana na usiku. Madini mengi yalikuwa yakipatikana kila siku na kusafirishwa kupelekwa nje ya nchi.
Bado makampuni mbalimbali ya uchimbaji madini yaliendelea kuongezeka mgodini hapo hali iliyowavutia zaidi vijana kumiminika mgodini hapo. Hakukuwa na mtu aliwajali watoto, watoto mbalimbali walikuwa wakiajiriwa mgodini hapo kwa ajili ya kuchekecha mchanga wa almasi ambazo zilikuwa zikichimbwa kila siku.
Malipo yalikuwa yakifanywa vizuri kiasi ambacho kila mtu alionekana kuridhika. Huduma mbalimbali za kijamii zilizidi kuongezeka katika Mji wa Mwadui kiasi kwamba hadi watu kutoka mikoa mingine ya jirani kutamani kwenda kuishi katika mji huo ambao ulikuwa ukizidi kuendelea kila siku.
Patrick alikuwa mmoja wa watoto ambao walikuwa wameajiriwa katika kampuni ya uchimbaji madini iliyokuwa mahali hapo ambayo iliitwa MWAGOCO DIAMOND COMPANY LIMITED. Kila siku kazi yake pamoja na watoto wengine ilikuwa ni kuchekecha mchanga ambao ulikuwa umechimbwa katika mashimo mbalimbali.
Kila siku mashimo ya kampuni ya MWAGOKO yalikuwa yakitoa almasi nyingi kuliko mashimo yote yaliyokuwa katika mgodi huo wa Mwadui. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifahamu kitu chochote kuhusu siri iliyokuwa imeufunika mgodi huo.
Kila siku magari mbalimbali makubwa yalikuwa yakifika katika mgodi huo hasa karibu na mashimo ya kampuni ya MWAGOKO na kuchukua mchanga ambao tayari ulikuwa umechekechwa. Kampuni ya MWAGOKO ikawa kampuni pekee iliyokuwa na wafanyakazi wengi ambao walikuwa wakilipwa vizuri kuliko kampuni zote mgodini hapo.
Kwa miezi miwili ambayo Patrick alikuwa ameishi mgodini hapo, hakuzoeana na mtu yeyote zaidi ya Aziz, mtoto ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja naye. Kila wakati walikuwa pamoja, chakula walikula pamoja na hata sehemu walilala katika hema moja.
Walizoeana kupita kawaida kiasi kwamba kila mtu alijua watoto hao walikuwa ndugu. Kitu kilichoonekana kuwa tofauti kwao ni rangi tu. Aziz alikuwa mchanganyiko wa rangi mbili, Kiarabu na Mswahili huku Patrick akiwa Mswahili kamili.
Kila siku walikuwa wakifanya kazi pamoja katika Kampuni ya MWAGOKO iliyokuwa chini ya Bwana Mayasa Godfrey, tajiri ambaye alikuwa akimiliki mali zilizokuwa na kiasi cha shilingi Trilioni kumi.
Hakukuwa na mtu ambaye hakuwa akimfahamu Bwana Mayasa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kila siku utajiri wake ulikuwa ukiongezeka, alinunua magari ya kifahari pamoja na nyumba kubwa za kifahari. Fedha kwake haikuwa tatizo kabisa, alitumia fedha kwa kadri alivyoweza lakini wala hazikupungua zaidi ya kuongezeka kila siku.
Mbali na mafanikio ya kampuni hiyo, kulikuwa na siri kubwa nyuma yake, siri ambayo hakukuwa na mtu yeyote aliyeifahamu.
Damu za watoto ndizo zilizokuwa zikitumika katika katika mashimo yaliyokuwa yakimilikiwa na kampuni ya MWAGOKO. Kila wiki watoto walikuwa wakichukuliwa kutoka mitaani na kupelekwa katika migodi hiyo ambako walichinjwa na damu zao kunyunyiziwa katika sehemu mbalimbali.
Majini ndiyo yaliyokuwa yakinywa damu hizo ambazo zilikuwa zikinyunyiziwa na kisha kuruhusu almasi nyingi kupatikana katika mashimo hayo. Ukatili uliokuwa ukifanyika mara kwa mara haukuwa ukijulikana na mtu yeyote zaidi ya Bwana Mayasa na wafanyakazi wake wa karibu ambao alikuwa akiwaamini kupita kiasi.
Watoto walikuwa wakipotea mitaani, wazazi walikuwa wakiwatafuta katika kila kona lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yale. Walikuwa wakiingizwa katika buti za magari na kisha kusafirishwa kupelekwa katika migodi hiyo pamoja na baharini.
Kila mwaka zaidi ya watoto elfu kumi walikuwa wakipotea mitaani na kupelekwa katika migodi mbalimbali pamoja na baharini kwa ajili ya kutolewa kafara. Kila siku Serikali ilikuwa ikijitahidi kwa nguvu zote kutaka kujua sehemu ambayo watoto hao walipokuwa wakipelekwa lakini hakukuwa na mtu aliyepata jibu.
“Unasemaje?” aliuliza Bwana Mayasa huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Ndiyo hivyo mzee. Yaani tumejitahidi sana, hatujafanikiwa,” ilisikika sauti ya upande wa pili.
“Haiwezekani. Yaani watoto wote huko!”
“Ndiyo hivyo mzee. Kila mzazi amekuwa makini na mtoto wake, au kama utatupa wiki moja tujitahidi,” sauti ile iliendelea kusikika.
“Wiki moja! Acha utani. Tunataka tuanze kazi leo usiku wewe unaniambia baada ya wiki moja! Naona umechoka kazi Stefano,” alisema Bwana Mayasa huku akionekana dhahiri kuchaganyikiwa mno.
“Lakini bosi h...” sauti ya Stefano ilisikika lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake, mzee huyo akakata simu kwa hasira.
Bwana Mayasa akachanganyikiwa. Amani ikatoweka moyoni mwake, aliwaona vijana wake kutofanya kazi aliyotaka ifanyikie haraka iwezekanavyo. Watoto walihitajika haraka sana kwa ajili ya kuwachinja na damu zao kutumika kama sadaka katika mashimo yake, kukosekana kwa watoto hao kulimaanisha kwamba sadaka isingetolewa na hivyo basi majini kukasirika na kuyaficha madini
Kikao cha dharura kikaitishwa ndani ya chumba kimoja kidogo, muda wote Bwana Mayasa alionekana kuwa na hasira. Tayari aliyaona mambo kuanza kwenda kombo, kila wakati alikuwa akipiga meza kwa hasira. Wafanyakazi wake wa siri ambao walikuwa mahali hapo wakaogopa, hawakuwahi kumuona mzee huyo akiwa katika hali hiyo hata siku moja.
“Usikasirike mzee. Ni lazima tufaye kitu fulani,” alisema Godwin, mfanyakazi ambaye alikuwa akiaminika sana na Bwana Mayasa alimwambia huku watu wote wakiwa kimya kumsikiliza.
“Kitu gani? Unafikiri kitu gani ambacho tunatakiwa kufanya?”
“Kwani si hata hapa Mwadui kuna watoto. Kwa nini tusiwachukue hata hao. Tena wapo watoto wengi kweli,” alisema Godwin.
Bwana Mayasa akaonekana kama kushtuliwa katika lindi fulani la mawazo, akamwangalia Godwin, tabasamu pana likaanza kuonekana usoni mwake. Wazo hilo likapitishwa kwa nguvu zote, vijana watatu ambao walitakiwa kufanikisha kwa kazi hiyo wakaandaliwa kwa ajili ya kazi kufanyika usiku wa siku hiyo.
Je, nini kitaendelea?

Post a Comment