Serikali Yakana Kumshikilia Yusuf Manji
Sakata
la kushikiliwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Yusufu Manji
limeendelea kuchukua sura mpya, safari hii yakiibuka mabishano Mahakama
Kuu baada ya Serikali kukana kumshikilia.
Mabishano
hayo yameibuka jana kati ya mawakili wa Serikali na mawakili wa Manji
baada ya mfanyabiashara huyo kufungua maombi juma lililopita akihoji
uhalali wa kushikiliwa na Uhamiaji.
Manji
aliyefungua maombi hayo mahakamani hapo kupitia Wakili wake Hudson
Ndusyepo, anaiomba mahakama iiagize Uhamiaji afikishwe mahakamani ili
mahakama iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kisha iamuru aachiwe
huru.
Kutokana
na maombi hayo, Jaji Ama-Isario Munisi, aliwaamuru wajibu maombi
kuwasilisha hati zao za kiapo kinzani dhidi ya maombi hayo na kupanga
kuyasikiliza jana mchana.
Wajibu
maombi ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es
Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam.
Hata
hivyo jana Serikali katika majibu yake kupitia hati ya kiapo kinzani
cha Ofisa Uhamiaji, Anorld Munuo, ilikana kumshikilia mfanyabiashara
huyo. Mbali na kiapo hicho, Wakili Mkuu wa Serikali, Oswald Tibabyekoma,
alisisitiza kuwa mfanyabiashara huyo hashikiliwi na yuko huru.
Post a Comment