Mbunge wa Nzega Hussein Bashe Afunguka Maneno Mazito Kuhusu Hali ya Kisiasa Ilivyo Hivi sasa Nchini
"Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu.
"Msikubali
kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya
kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru.
"Ni
jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje
ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa
au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu.
"Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu.
"Kwa
kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia
katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania UHURU wa
taifa letu. TUJISAHIHISHE."
Post a Comment