KUTOKA LUSAKA, ZAMBIA.....ZANACO 0 VS YANGA 0 (FULL TIME)-ZANACO WANASONGA MBELE KWA FAIDA YA BAO LA UGENINI
ZANACO WANAFUZU KWA FAIDA YA BAO LA UGENINI BAADA YA SARE YA 1-1 JIJINI DAR ES SALAAM
-Krosi nzuri ya Kessy, Mwinyi anauwahi mpira na kuachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango
-Yanga wanapata kona, Dida anakwenda kwenye lango la Zanaco. Inachongwa lakini hakuna kitu
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Mwinyi anajaribu shuti kali kabisa hapa lakini kipa anadaka kwa ufundi
Dk 88, kona nyingine ya Lyanga almanusura mpira uingie wenyewe lakini inakuwa goal kick
Dk 86 kona ya Lyanga aliyoichonga vizuri lakini Mwinyi anafanya kazi ya ziada kuokoa na kuwa kona tena
Dk 85, Lyanga anamuacha Kamusoko lakini Yondani anakuwa makini, anaokoa na kuwa kona
KADI Dk 84, Kwame wa Zanaco na Bossou wanalambwa kadi ya njano kila mmoja baada ya kusukumana sukumana
Dk 80, kipa Tostan wa Zanaco anaudaka mpira laini kabisa wa krosi ya Kessy, lakini anajiangusha na kubaki chini hali inayoashiria Zanaco wameanza kupoteza muda kijanja
Dk 78, kona safi ya Niyonzima, Martin anapiga kichwa lakini Kamusoko anaangushwa na kuwa faulo
Dk 78, Chirwa anawachachafya mabeki wa Zanaco, wanatoa inakuwa kona
Dk 77, Taonga anaachia mkwaju mkali katika mpira wa faulo, nje
KADI Dk 75, Mwinyi analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Musonda
Dk 72, Yanga wanagongeana vizuri na Martin anaachia shuti kali hapa lakini goal kick
Dk 69, shuti kali la Msuva linatoka sentimeta chache. Hata hivyo angeweza kutoa krosi ingekuwa poa zaidi
SUB Dk 65 Zanaco wanamtoa Mulenga wanamuingiza Ayoub Lyanga, kija Mtanzania aliyejiunga na Zanaco akitokea African Sports ya Tanga
Dk 62, Mwinyi Haji na Kessy wanagongana wakati wakiiwahi krosi ya MSuva
Dk 59, Kessy anagongeana vizuri kabisa na Emmanuel lakini krosi yake inatoka nje kidogo
Dk 56, kidogo Niyonzima na Kamusoko wanaonekana kuonana vizuri lakini hakuna mipira ya hatari langoni mwa Zanaco
SUB Dk 54 Moyo anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Kasonde kwa upande wa Zanaco
Dk 53, Msuva anageuka na kuachia mkwaju hapa lakini Moyo anaweka mguu wake, faulo
Dk 53, krosi ya nguvu ya Haji Mwinyi lakini Chirwa anachelewa kidogo tu
SUB Dk 52, Yanga wanamtoa MWashiuya na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 51, Yanga wanapata kona ya kwanza katika kipindi cha pili baada ya Taonga kuutoa mpira nje akimdhibiti MWashiuya
Dk 49, shuti kali la Taonga, mpira unazunguka lakini Dida anaokoa mpira unatua miguuni mwa Musonda ambaye anaachia shuti kuuuuubwaaaaaa, goal kick
Dk 47, krosi safi ya Haji Mwinyi, inakosa mwenyewe ndani ya lango la Zanaco
Dk 46, Sakala tena akiwa na kipa Dida anashindwa kutulia na kutoa nje, goal kick
Dk 45, Zanaco wanaingia vizuri lakini shuti la Sakala linatoka sentimeta chache
MAPUMZIKO
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45 MWinyi Haji anafanya uzembe na kutoa pasi fupi, Kwake anauwahi na kutaka kufunga lakini Dida anaokoa. Ilikuwa hatari
Dk 44, Mulenga tena anaachia mkwaju lakini Yanga wanaokoa
Dk 43, Mulenga aliwachambua mabeki wawili wa Yanga lakini Yondani akakaa imara, akamgeuza na kuchukua mpira
Dk 42, Zanaco wanaingiza majaro safi kabisa lakini Zulu anakuwa mwepesi na kuokoa
Dk 39, Zanaco wanachonga kupitia Mulenga, Moyo anapiga kichwa lakini ni goal kick
Dk 38 Moyo anaachia shuti kali mpira wa adhabu, Dida kwa umahiri mkubwa anaokoa na kuwa kona
KADI Dk 37 Yondani anamuangusha Sikala na mwamuzi huyu kutoka Kenya, anampa kadi ya njano
Dk 35, Haji Mwinyi anaachia mkwaju mkali kwelikweli akiwa umali wa takribani mita 30, lakini unatoka juu ya lango sentimeta chache
Dk 31, nafasi nzuri ya kupiga shuti lakini Kamusoko anaamua kutoa pasi inawahiwa na Tossa na kuokoa
Dk 30 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja. Kinachoonekana kumekuwa na umakini mkubwa katika safu za ulinzi kwa kila upande
Dk 28, Yondani yuko chini akigaagaa pale. Nafikiri ni maumivu
Dk 27, Zanaco wanapata kona nyingine na inachongwa na Mulenga....Dida anapangua vizuri na Kessy anaosha mbali kabisa
Dk 26, Msuva anaichonga vizuri kona fupi, kwake Niyonzima anaimimina lakini unaokolewa
Dk 25, Chirwa anaingia vizuri lakini mpira unaokolewa na kuwa kona
Dk 21, kona nyingine ya Zanaco inaokolewa na kuwa mpira wa kurushwa
Dk 20, Zanaco wanapata kona, inachongwa vizuri kabisa lakini anaokoa Bossou.
Mechi sasa ni dakika ya 15, bado kila upande unashambulia kwa zamu na hakuna timu iliyopata bao.

HINTS:
Katika mechi ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya mabao 1-1kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi ya leo, Yanga inaweza kufuzu kwa sare ya mabao 2-2 na kuendelea. Au ushindi wa aina yoyote.
Post a Comment