GWAJIMA AMUUMBUA MWANASHERIA ALIYEJIITA NDUGU YAKE.!
Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Dr.Josephat Gwajima, amesema Mwanasheria Methusela Gwajima ambaye alijitambulisha kuwa mdogo wake, si mdogo wake wa kuzaliwa, wala si mtoto wa ndugu yake isipokuwa ni ndugu wa ukoo.
Askofu Gwajima amesema Methusela (ambaye jina lake halisi ni Joshua) ni kada wa muda mrefu wa CCM na amewahi kuwa Katibu wa CCM wilaya ya Singida na baadae wilaya ya Nzega mkoani Tabora. Pia amesema kuwa Methusela si mwanasheria maana ameghushi vyeti vyake vya taaluma, na kama asiponyamaza ataweka taarifa zake hadharani.
Askofu Gwajima ameongeza kuwa Methusela hana uhalali wa kumtetea Makonda kwasababu ana conflict of Interest, maana wote wamekua viongozi wa CCM katika nyadhifa tofauti.!
Nini maoni yako??

Post a Comment