Godbless Lema Asimulia Maisha ya Gerezani na Jinsi Alivyopewa Cheo cha Nyapara Kuwaongoza Wafungwa Wenzake
Aidha,
amesema akiwa katika mahabusu hiyo, alipewa cheo cha nyapara na kuweza
kuwaongoza wafungwa wenzake, jambo lililomfanya kufahamu matatizo na
manyanyaso mbalimbaliwa, wanayofanyiwa wafungwa.
Lema
alisema hayo katika Viwanja vya Ngarenaro jijini Arusha jana, alipokuwa
akiwahutubia wakazi wa jimbo lake katika mkutano wa hadhara.
“Kwani
nimekosa nini? Kutoa maoni ndio nifanywe hivi kweli? Nilikuwa naomba
sana kwa Mungu tangu nilipowekwa ndani hadi siku nilipotoka.
“Na
Mungu aliniambia endelea kuomba na usubiri uone miujiza yangu, lakini
akaniambia wasamehe wote waliokukosea kwa kukuweka gerezani bila kosa.”
Akizungumzia kosa alilolifanya la kutoa kauli ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli; Lema alisema; “Nilivyosema
nimeona maono walidhani mimi ni kichaa, lakini Mungu ndiye
atakayethibitisha maono haya, kama yalikuwa ni feki au la.
“Dhambi
mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni uoga, kinachotesa nchi hii si
polisi, ni uoga, angalia kilichotokea juzi mahakamani, nimekaa ndani
miezi minne halafu nilipotoka wananchi walikamatwa na kupigwa, kisha
wakafunguliwa kesi ya mkusanyiko usio halali, jambo ambalo ni la
uonezi,” alisema Mbunge huyo.
Akitoa ushauri kwa polisi, Lema alisema; “
Nawaomba polisi muwe na utu, kwani damu mnayoimwaga itawarudia, hakuna
dhambi itakayopandwa ikavuna haki, kwanini mnawapiga watu? Nasema Mungu
yupo.”
Alisema
Idara ya Mahakama, haipo huru na kwamba kielelezo cha Serikali
kuingilia mhimili wa mahakama ni hatua ya hivi karibuni ya Rais Magufuli
kumteua Kaimu Jaji Mkuu badala ya Jaji Mkuu.
Alisema
lengo la uteuzi huo, aliodai si sahihi, ni kuifanya Serikali icheze na
sheria na kwamba tafsiri iliyo ni kuilazimisha Mahakama icheze wimbo wa
serikali.
“Hili
ni jambo la hatari sana, kwani watu wakijua kuwa Mahakama inayumbishwa
na haijasimama imara, haki itatafutwa mitaani. Mateso niliyoyapata
Magereza, yamenitengeneza kuwatetea waliopo magerezani.
“Nakuomba
Mbunge mwenzangu James Millya (Mbunge wa Simanjiro – Chadema), tukienda
bungeni turekebishe sheria, maana tulipozitunga, tulidhani sisi
haitugusi kumbe inatugusa, hivyo tuombe ifanyiwe marekebisho.”
Alisema
pia akiwa jela, alishuhudia mambo mbalimbali, ikiwemo kufungwa kwa
vijana wadogo wenye umri wa miaka 14 kinyume cha sheria za nchi.
Aliongeza; “Umri huo ni mdogo sana na ninaposema Magereza, lazima mjuwe hali halisi iliyopo magereza."
Alisema
pia alishuhudia kuwekwa mahabusu kwa watu wengine kwa muda mrefu, bila
kufikishwa mahakamani au kupewa dhamana, jambo alilosema ni kukiuka
sheria za nchi.
Alisema
kutokana na uzoefu alioupata mahabusu kwa kipindi cha miezi minne,
anaandika kitabu kuhusu wafungwa wanavyoteseka magerezani.
Alisema
pia akiwa mahabusu, ameweza kukutana na watu wanaoitwa magaidi zaidi ya
65 wakiwa wamekaa kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka minne; huku wengine
wakiwa wamekatwa miguu, lakini cha ajabu ni kuwa hawajahukumiwa
kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi.
“Unapochelewesha
kesi za ugaidi, unajenga tabaka kati ya dini na dini, kama ni magaidi,
malizeni upelelezi ili wahukumiwe, lakini kwa upelelezi wangu na
uchunguzi wangu sijaona kama hao watu ni magaidi.
“Natoa agizo, mmalize upelelezi kabla sijaenda Bungeni, hii haitakuwa noma ndogo, itakuwa noma kubwa nikienda Bungeni.
“Kama
mimi Mbunge mmeninyima dhamana, kila siku mnaweka mapingamizi narudi
gerezani, hali ikoje kwa watu wasioandikwa kwenye magazeti ambao
hawajulikani, ni wazi kuwa wananyanyaswa sana,” alisema mbunge huyo.
Kabla
ya kuanza kuhutubia, Lema alimpa nafasi msanii, Wema Sepetu ambaye
alimtaja kuwa ni mwanamke jasiri na kuwa ana uhakika atashinda katika
kesi yake ya kudaiwa kukutwa na dawa ya kulevya.
Akihutubia,
Wema alisema ana imani na Mungu na kuwa mitihani ya maisha,
anayokumbana nayo ni mipango ya Mungu katika kumfikisha mahali alipo
hivi leo.
Alimuomba Lema kusamehe kila analofanyiwa na kutolipiza kisasi ili kupata baraka za mwenyezi Mungu.
Naye,
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini, Derick Magoma alisema
Chadema wilaya Arusha, ipo imara haijayumba wala kutetereka wakati Lema
alipowekwa mahabusu kwa kipindi cha miezi minne.
“Hatumpi
mtu yoyote kura, bali ni Lema hadi 2020 au zaidi ya hapo, tumefanya
maendeleo kwa kipindi cha miaka miwili na wananchi wote mnajua kuwa
maendeleo yameletwa na Chadema” alisema.
Meya
wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, alieleza furaha aliyonayo kutokana na
kitendo cha kuachiwa kwa Lema. Alisema kwamba miezi minne aliyokaa
mahabusu, si jambo la mchezo.
“Mbunge
najua walikuweka ndani sababu ya kudhoofisha maendeleo ya Jiji la
Arusha, lakini kwa sababu una Meya na madiwani bora wa Baraza la
Madiwani, hatukuweza kutetereka” alisema Lazaro.
Post a Comment