CONTE SI MTU WA KUJIVUNGA, AELEZA WAZI KUMTAKA SANCHEZ
Bosi
wa Chelsea, Antonio Conte si mtu wa kujivunga hata kidogo, tayari
ameweka hadharani kwamba anamtaka mshambuliaji Alexis Sanchez.
Sanchez ameeleza wazi kwamba anataka kuondoka Arsenal ingawa hajasema anakwenda wapi.
Lakini ajabu, Arsenal inaonyesha haitaki kumuuza London kwa Chelsea au England kwa timu yoyote.
Badala yake, Arsenal inaamini Sanchez anapaswa kuuzwa nje ya England.
Conte
anaamini, baada ya Chelsea kubeba ubingwa kama mambo yataenda safi hadi
mwisho, bass Sanchez atakuwa msaada mkubwa hapo baadaye.
Post a Comment