Waziri Nape aingilia kati sakata la wasanii wanaotuhumiwa kwa Madawa ya Kulevya, Ataka Busara Itumike
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia kati na
kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika na dawa
za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Nape
ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari
kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku nne tangu mkuu
huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya wakiwemo wasanii
wa bongo fleva na filamu.
Baadhi
ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja na
Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda, Babuu wa
Kitaa n.k
Nape
baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu suala hilo amesema kuwa
wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya
kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C
na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.
Amesema
tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia dawa za
kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia tatizo
lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao tayari
wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.
Kwa
mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri
jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.
Post a Comment