Profesa Lipumba Akanusha Kuwa 'Kibaraka' wa Serikali
Mwenyekiti
wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekanusha tuhuma
za kuwa na ukaribu unaotia shaka kati yake na serikali na kutolea
ufafanuzi ishu mbalimbali zinazoashiria ukaribu huo ikiwemo ya
kuchepusha ruzuku ya chama.
Mwenyekiti
huyo anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kinachodaiwa
kuwa ni ukaribu wake na serikali, siyo sahihi kwa kuwa yeye huwa
anaalikwa tu kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa ambayo hawezi kukataa
mwaliko.
"Kwa
mfano ukikaribishwa kwenye shughuli ya serikai, labda Rais anazindua
kitu, au sherehe za kitaifa na Rais yupo utakataaje" Amesema Lipumba.
RUZUKU
Suala
la ruzuku ya chama hicho kuchepushwa pia ni jambo linalodaiwa kuwa
ushahdi wa Prof Lipumba kuwa karibu zaidi na serikali, ambapo amesema
ilikuwa ni lazima iwe hivyo kutokana na uamuzi wake kama Mwenyekiti wa
chama wa kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Fedha, ambaye ndiye aliyekuwa
mtia sahihi katika masuala ya fedha.
Pia
sababu nyingine ya kuchepusha fedha za ruzuku amesema ni mahitaji ya
chama kwa kuwa kilikuwa kinaingia kwenye uchaguzi hivyo kilihitaji fedha
kwa ajili ya shighuli mbalimbali.
"
Kuhusu ruzuku, nilikuwa nimetengua uteuzi wa mkurugenzi wa fedha, bwana
Bashange, kwahiyo hakuwa tena signatory wetu, kwa nafasi yangu kama
mwenyekiti niliona hafai, tukajitahidi kufungua akaunti nyingine lakini
haikuwezekana. Ikabidi Naibu Katibu Mkuu ambaye ndiye anayeshika nafasi
ya Katibu Mkuu anapokuwa hayupo ofisini, aandike barua ya kuomba ruzuku
kwa ajili ya mahitaji tuliyokuwa nayo" Ameeleza Lipumba
Lipumba ameendelea kusema "Tukapeleka
taarifa kuomba ruzuku. Kwahiyo Naibu Katibu Mkuu akaandika barua kwenda
kwa Msajili kuwa tunaomba ruzuku na ipitie kwenye akaunti nyingine, na
hilo likafanyika"
MIKUTANO
Kuhusu
yeye kuruhusiwa kufanya mikutano, huku Katibu Mkuu wake akizuiliwa,
hususani tukio lililotokea mkoani Mtwara, Lipumba amesema hata yeye
alipokwenda Mtwara hakuruhusiwa kufanya kilichokuwa kimempeleka, na
badala yake aliishia kufanya mikutano ya ndani, huku akibainisha kuwa
kilichomkwamisha Maalim Seif ni kwenda bila kutoa taarifa kwa kiongozi
wa wilaya.
"Nimekwenda
Mtwara, nilikaribishwa na viiongozi wa wilaya, kazi yangu ilikuwa ni
kufungua matawi, lakini polisi wakanizuia kuwa sitakiwi kufanya mikutano
ya nje, nikafanya mikutano ya ndani...Lakini Maalim Seif alikwenda bila
kumtaarifu kiongozi wa wilaya". Amesema
ULINZI
Lipumba
aliyekuwa katika mahojiano na kituo kimoja cha TV, amekanusha taarifa
za kupewa ulinzi na serikali na kufafanua tukio la kupigiwa saluti na
askari, akisema kuwa siku hiyo hakupigiwa yeye saluti bali diwani wa
eneo ambalo yeye alishiriki kufanya usafi.
"Pale
Buguruni, tulikuwa katika usafi, na tulikuwa na diwani wa eneo lile,
askari walikuwa wakiangalia usalama, na alipotokea diwani wa eneo lile,
askari walimpigia yeye kwa kuwa ndiye mkuu wa eneo lile, siyo mimi"
Kitendo kilichodaiwa kuwa ni askari kumpigia saluti Prof Lipumba
Katika
hatua nyingine, amesema anaendelea kumtambua Maalim Seif kama Katibu
Mkuu halali wa CUF, huku akimtaka amfuate ili wamalize tofauti zao na
kufanya kazi kwa pamoja.
Post a Comment