TASWIRA NNE MAKAMU MWENYEKITI YANGA ALIVYOTUA SENTRO, MANJI AKIENDELEA KUBAKI NDANI
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amefika katika kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani
Dar es Salaam kwa tuhuma za suala la madawa ya kulevya zilizotolewa na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Sanga alifika kituoni hapo na kupitiliza moja kwa moja lango la ukaguzi na baadaye alienda lango kuu la kuingilia ndani.
Haijajulikana mara moja, alikuwa akifanya nini zaidi ni kwenda kumuona mwenyekiti wake anayeshikiliwa tokea jana.
Baada
ya kutoka, Sanga hakutaka kuzungumza lolote lakini imeelezwa amekuwa
akishughulikia masuala kadhaa ya kisheria pia kuhakikisha timu inasafiri
kwenda Comoro kwa kuwa Manji ambaye ni kiongozi mkuu yuko mahabusu na
yeye ndiye hushughulikia masuala ya fedha hasa suala la uidhinishaji.
“Sanga
alikwenda kumjulia hali Manji. Lakini lazima watakuwa wamejadili
masuala ya klabu. Hawezi kuyazungumzia hayo hadharani,” kilieleza
chanzo.
Post a Comment