Kauli ya Vanessa Mdee Baada ya Kutajwa na RC Makonda Kwenye Listi ya Wahusika wa Madawa ya Kulevya
Iliwashangaza
wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na biashara ya
madawa ya kulevya.
Ni shutuma nzito, na hata kabla uthibitisho rasmi haujatoka, madhara ya kutajwa majina yao yameanza kuonekana katika maisha yao.
Wito
huo umemkutia Vee Money akiwa nchini Afrika Kusini anakoshoot tamthilia
ya MTV Shuga, na bila shaka atalazimika kukatisha kwa muda na kurudi
Tanzania kwenda kituo cha polisi central, anakotakiwa Jumatatu ya kesho.
Pamoja
na hivyo, Vee ameonesha kuvuta pumzi ndefu na kuacha maisha yaendelee
kama yalivyo. Kupitia Instagram, Vee amepost picha hizo juu na katika
ile aliyokaa ameandika: The show must go on … bomb ass dress from @asos #FILA.
Kwenye hiyo black and white ameandika: The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.”
Post a Comment