PRESHA YA SIMBA YAWASHANGAZA YANGA, WATABIRI KUITWANGA MABAO MZIGO
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga amesema, wanaamini watawafunga nyingi Simba kutokana na presha yao.
"Hawa jamaa wanajipa pesha sana nakuambia, unajua ungebahatika kwenda kwenye kambi ya Yanga ungeshangaa sana.
"Watu
wako kikazi na hakuna presha. Wachezaji wanaendelea na mambo yao vizuri
na hakuna presha kabisa. Sasa wenzetu sijui wana nini, utafikiri
wakishinda kesho, wanatangazwa mabingwa na kupewa kombe!" alisema.
Mechi
hiyo itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
inaonekana kuzidi kuwa na presha huku kila upande ukiogopa kupoteza.
Post a Comment