Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul anusurika Kifo, Alazwa ICU, Ziara yaahirishwa

Mbunge
 wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari 
lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya 
ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira 
Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Baada
 ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati 
mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba 
cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika 
chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo 
Hata
 hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika 
kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa 
babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua
 umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari
 kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.
Post a Comment