Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe, Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo
Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru
atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji kumhoji.
Kamanda
wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe
kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda.
Amesema
operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa
hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na
wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani
taarifa imeshatolewa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.
Post a Comment