ad

ad

Wema Sepetu aibuka upya Instagram, Atupia picha Amazing






MREMBO asiyeishiwa matukio kila kukicha Bongo, Wema Isaac Sepetu hatimaye ameibuka kwa mara nyingine kutoka mafichoni alikokuwa amejificha kwa muda mrefu, baada ya kuitelekeza kwa muda akaunti yake hiyo ambapo kwa  kufuta picha zake zote za zamani na kubakiza masualia mengi kwa mashabiki wake ambao hawakuweza kupata majibu yake.
Kabla ya kufuta kila kitu kwenye akaunti yake hiyo, Wema alikuwa na zaidi ya followes Milioni mbili na nusu, ambao wameendelea kumvumilia hadi jana jioni aliporejea na kuanza kuweka picha mpya kwenye profile yake kisha akaipost upya kwenye akaunti yake hiyo.

Hadi muda huu Wema bado hajatoa sababu ya msingi iliyomfanya aamue kufuta posti zake hizo pamoja na kuwa na maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake wakimtaka awafafanulie kilichomfanya kuchukua uamuzi huo.
Wema amerudi na mafumbo makali ambayo yanaonekana kutowaweka wazi mashabiki zake kwani hadi muda huu ameandika ujumbe unaosomeka kuwa....
Happy 2017... and am excited.. how Many Likes?? Share from
This one and am gonna Tell You something to Celebrate for the whole Year.... #WSSoCloseToYou #WSladieschoice #WSyourAddiction
#unataka kusikia jambo zuri kutoka kwangu kwa mwaka 2017? Gonga Likes za kutosha and nitarudi kukung'ata sikio... This be your First Image.... There is plenty of these Just for You.... I missed You too.... @ossegrecasinare You are Life....🤗

No comments

Powered by Blogger.