WEMA, KAJALA, UWOYA WAMEKUMBUKA SHUKA KUMEKUCHA
KIPINDI cha nyuma mastaa wengi wakubwa wa filamu nchini walikuwa wakibweteka huku wakiwa hawana muda kabisa wa kujishughulisha na kitu chochote wakati walikuwa wanahitaji kuvaa nguo nzuri za gharama, kuendesha magari mazuri na kuishi nyumba nzuri huku wakiwa hawana kitu chochote cha kuwaingizia kipato cha ziada.
Wengi wa mastaa hao ambao kikubwa walikuwa wakitegemea filamu ambazo wanazitoa mara moja kwa mwaka na malipo yao ni kulipwa kwa awamu kitu ambacho kilikuwa ni kigumu kabisa kukidhi mahitaji yao ya kila siku huku wengi wao wakiwategemea mapedeshee kuwaendeshea maisha yao. Katika kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano, mambo yamebadilika.
Mastaa wengi wameamua kupiga mzigo bila kujali majina yao wala kuangalia ni nani atawacheka au atajadiliwa vipi ndipo baadhi mastaa wa kike wenye majina makubwa Bongo Muvi, wakaamua kujichanganya kwenye kusaka ‘chapaa’. Mastaa hawa wanaendana kabisa na msemo usemao wamekumbuka shuka wakati kumekucha kwa sababu wamechelewa, wangeanza mapema sasa hivi wangekuwa mbali sana:
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja-x5KpQusjyoWR8wjI_vCVeYgrWiQCZlCT0VFVku3dHoaprNb2putfYwSfRr5XUTDDLadyuN05VQJpOzyu2MiZtNmTC1BUb_Ad1dBpHCUVU-4-C0FbEJHltU9mGFLCI8KeiDjpYSuUWk/s640/wema.jpg)
WENGI walijua wazi staa huyu ambaye anafanya vizuri kwenye fi lamu kutokana na maisha ambayo alikuwa akiishi asingeweza kabisa kufi kiria kufanya biashara yoyote ya kumuingizia kipato kutokana na maisha aliyokuwa akiishi nyuma lakini sasa hivi ameamua kujiingiza kwenye ujasiriamali kwa kuuza sabuni ya kufulia na kufanya usafi majumbani.
“Kwa sasa hakuna maisha bila kujishughulisha, nilikaa na kuamua sasa ni kipindi cha kujituma zaidi bila kusubiri kuletewa na mtu yeyote na ninashukuru sasa hivi nauza sabuni ambayo natengeneza mwenyewe kwa mikono yangu na mambo yanaenda sawa kabisa,” anasema Kajala.
AUNT EZEKIEL
STAA huyu hakuwa na tatizo kubwa sana huko nyuma kwenye kuitafuta njia mbadala ya kujikwamua kimaisha badala ya kusubiria malipo ya fi lamu kwani alishawahi kufungua baa mara mbili na kufunga lakini hivi karibuni alibuni mbinu mpya ya kuuza sabuni za kuogea zinazoondoa vipele alizozipa jina la Murua, ambazo mpaka sasa zinamsogeza sana kimaisha.
“Nadhani nyuma tulikuwa tunabweteka sana, tulitegemea sana kuletewa na kupewa, kitu ambacho tulikuwa tukikosea sana kwa sababu mimi nimejaribu na nimeweza na ninajilaumu nilichelewa wapi muda wote,” anasema Aunt.
UWOYA
KIPINDI cha nyuma jina la staa huyo lilikuwa kubwa sana lakini akajisahau kabisa kutumia jina lake kipindi kile kufanya vitu vyake muhimu vya kujikwamua kimaisha lakini sasa hivi naye ameamka na kuamua kuwa mjasiriamali kwa kufungua maduka mawili ya kuuza nguo na ushonaji kitu ambacho hawezi kulala njaa tofauti na mwanzo alivyokuwa akisubiria pato la filamu au kupewa na mtu.
“Hakuna hela nzuri kama ya kwako mwenyewe kwanza inakupa amani sana na hata wakati wa kuitumia maana unajua unatumia kitu ambacho umekitolea jasho pia ni heshima kubwa kwa mwanamke kutafuta hela mwenyewe, kusubiri za mtu ni kazi sana,” anasema Uwoya.
WOLPER
KATIKA mastaa waliokuwa na bahati kipindi cha nyuma, huyu ni mojawapo maana alikuwa na bahati ya kuwa kwenye uhusiano na wanaume wenye hela nyingi lakini matokeo yake hela haikuonekana ilipoishia. Mwisho alirudi kuhangaika kama zamani na wakati huo hakuwahi kuwaza kama anaweza kufanya kitu kikaweza kumsogeza kimaisha.
Hivi karibuni staa huyu ametambua thamani ya kujituma na kujibidiisha katika utafutaji wa hela kwa sababu ameamua kufungua sehemu ambayo anashona nguo mbalimbali za watu kitu ambacho kinampatia hela yake mwenyewe ambayo inampa heshima.
“Niliona kabisa umuhimu wa kukaa chini na kufi kiri ni kitu gani naweza kufanya na watu wakakifurahia pia nikatambua nina kipaji kingine kwa nini nisijaribu kufungua sehemu ya kushona nguo mbalimbali za akinamama hata wababa? Nimejaribu na ninaona wazi nimeweza,” anasema Wolper.
WEMA
UKUBWA wa jina la staa huyu ilikuwa ni njia tosha kwa wakati huu kuhesabiwa kama mmoja wa mastaa matajiri hapa Bongo kwani kwa kipindi cha nyuma angeweza kufanya kitu chochote kupitia jina lake na kuweza kubadilisha maisha yake lakini alishindwa. Hivi sasa kutokana na ugumu wa maisha ameamua kuanza kuuza viatu vyenye jina lake, na nywele ili kipato kiongezeke.
“Maisha ni magumu hakuna kumtegemea mtu yeyote, bidii yako ndiyo inayokuwezesha kula na ndivyo nilivyoamua kwa sasa hakuna hela rahisi bila kujituma hivyo siyo vitu pekee nitakavyofanya nitafanya vingi zaidi,” anasema Wema.
Post a Comment