TAARIFA YA UZUSHI KUHUSU MANJI KUSITISHA KUKODI TIMU YA YANGA YASAMBAZWA MITANDAONI, CHAMPIONI YAFAFANUA
KUNA
BARUA INAYOSAMBAZWA MITANDAONI, KWAMBA GAZETI LA CHAMPIONI LIMEFANYA
MAHOJIANO NA MWENYEKITI WA YANGA, YUSUF MANJI KUWA AMESITISHA
UKODISHWAJI WA TIMU NA NEMBO YA YANGA. HUO NI UZUSHI MTUPU NA GAZETI LA
CHAMPIONI HALIJAFANYA MAHOJIANO NA MANJI.
PIA
TUNATOA ONYO UPUUZI KAMA HUO WA KUSAMBAZA VITU VYA UZUSHI KWA KULITUMIA
GAZETI HILI. IWAPO TUTAMBAINI MTU, TUTAMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA.
MHARIRI
HABARI HIYO YA UZUSHI
MWENYEKITI
wa Yanga, Yusuf Manji, amesitisha kuendelea na zoezi la kuikodisha timu
na nembo ya klabu hiyo na kuwaambia wasaidizi wake, wasitishe mipango
yote ya maendeleo waliyokuwa wameanza kuifanya.
Manji
amewaambia wasaidizi wake kusitisha maandalizi ya Ligi ya Vijana ya
Matawi ya Yanga, lakini amewaambia waandae siku rasmi ambayo atazungumza
na vyombo vya habari na kuwaomba radhi Wanayanga ambao wamemuunga mkono
muda wote.
Habari
za uhakika ambazo Championi Jumatano limezipata, zinasema Manji
alizungumza na wasaidizi wake jana mchana ikiwa ni dakika chache baada
ya TFF kufanya mkutano na waandishi wa habari na kusema hawatambui suala
la Yanga kuikodisha timu na nembo kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd, kwa
miaka 10.
“Leo
alionekana ni kama mtu aliyekata tamaa au asiyefurahishwa na jambo.
Amewaita wasaidizi wake na wamefanya kikao, hakikuwa kirefu sana.
“Amewaambia ameamua kuachana na masuala ya kuikodisha Yanga, pia amesema ameona ni vizuri kuachana na masuala ya mpira.
“Kilichomuudhi ni wale wasiotaka mchakato wa mabadiliko Yanga, lakini hawatoi hoja za msingi,” kilieleza chanzo.
“Wasaidizi
wake walikuwa wameanza mchakato wa kutengeneza mfumo wa Ligi ya Vijana
ya Matawi ambao ungeigharimu Yanga yetu takribani Sh milioni 280 kwa
ajili ya vifaa, uendeshaji na kadhalika.
yangaaa-5
“Lakini
kuna suala amelizungumzia la uchaguzi, hilo sijaelezwa vizuri. Huenda
Yanga wakaitisha uchaguzi tena ili kuchagua viongozi yeye atakapotangaza
kujiuzulu rasmi.
“Anaweza
kufanya hivyo, yaani kutangaza kujiuzulu na kutangaza uchaguzi, pia
kuwaomba radhi wanachama na mashabiki waliomuunga mkono muda wote.”
Juhudi za kumpata Manji zilianza jana saa 7 mchana baada ya kupata taarifa hizi; lakini ilishindikana.
Mmoja wa wasaidizi wake alipopigiwa, alituma ujumbe mfupi: “Nipo kwenye kikao, nitafute baadaye.”
Alipopigiwa Manji saa 9 alasiri, akapokea, ilikuwa hivi:
Championi: Hallow
Manji: Nani mwenzangu?
Championi: Tunafuatilia kuhusiana na uamuzi wako wa kujiuzulu Yanga, tunataka kujua ni kwenye klabu au zoezi la kukodisha pekee.
Manji:
Tafadhali niacheni, kuweni kama binadamu. Nimechoka jamani, kuweni
waungwana na mimi ni binadamu. Mniache nipumzike (simu ikakatwa).
Yanga
Baadaye
mmoja wa wasaidizi wake alipiga simu akitaka kujua alikuwa anatafutiwa
kipi. Alipoulizwa suala la kujiuzulu kwa Manji, akasema:
“Sasa
ndugu yangu unataka kuniingiza matatizoni, nafikiri tuache atangaze
mwenyewe, naomba nipokee simu nyingine.” Kisha akakata simu.
Manji
ambaye aliiongoza Yanga kwa misimu minne, mitatu ikifanikiwa kuwa
bingwa Tanzania Bara, Kombe la FA na kucheza robo fainali ya Kombe la
Shirikisho, ndiye kiongozi kipenzi cha Yanga wengi hasa wanaovutiwa na
mafanikio ya timu yao.
Juhudi za kuendelea kumpata ili kuzungumza naye na kupata kila kitu kuhusiana na hili, zinaendelea.
Suala
la kutaka kuikodisha timu ndiyo limezua zogo, huku wachache wanaopinga
wakishindwa kuanika sababu hasa za msingi zinazowafanya wapinge.
Post a Comment