HII HAPA BARUA YA JERRY MURO KUOMBA MSAMAHA TFF YAVUJA....
Barua
ikimuonyesha Mkurugenzi wa Habari wa Yanga, Jerry Muro akiomba
kupunguziwa adhabu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imevuja
mtandaoni.
Barua
hiyo inaonyesha Muro aliandika Julai 7, mwaka jana akiomba kupunguziw
aadhabu ya mwaka mmoja baada ya kuutumikia kwa miezi sita.
Muro alifungiwa na TFF kwa mwaka mmoja kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Hivi
karibuni, Mkurugenzi wa kitengo cha habari cha klabu ya Simba, Haji
Manara alimuombea msamaha Muro na kuishauri TFF kumuondolea adhabu hiyo.
SALEHJEMBE, inamuunga mkono Muro kuomba radhi kwa kuwa ni sehemu ya uungwana wa mwanadamu kufanya jambo hilo.
SALEHJEMBE inaiasa TFF, kuliangalia ombi la Muro na ikiwezekana kulifanyia kazi kwa kumsamehe.
Post a Comment