Rais mpya wa Gambia kurejea nyumbani leo
Mai
Fatty msemaji wa rais Barrow ambaye amekuwa akiishi nchi jirani ya
Senegal alikoapishwa, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa
rais huyo mpya atarejea nyumbani ili kuanza rasmi majukumu ya kuliongoza
nchi hiyo.
Aidha, Fatty amesema rais Barrow anatarajiwa kuwasili jijini Banjul leo mchana akitokea jijini Dakar.
“Ndio, leo mchana atawasili,” Fatty ameliambia Shirika la AFP.
Barrow
aliyeshinda Uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita, alisema hawezi
kurejea nyumbani hadi pale atakapopewa idhini na jeshi la Umoja wa nchi
za Afrika Magharibi ECOWAS ambalo kwa sasa lipo jijini Bajul kuhakikisha
kuwa kuna usalama hasa katika Ikulu na makaazi ya rais.
Maelfu
ya raia wa Gambia ambao walikimbilia katika nchi jirani ya Senegal,
wameanza kurejea nyumbani baada ya Jammeh kuondoka wiki iliyopita.
Jammeh
alilazimika kuondoka nchini humo baada ya kutishiwa kuondolewa kwa
nguvu na jeshi la ECOWAS lakini pia baada ya marais wa Mauritania na
Guinea, kuingilia kati mzozo huo na kumshawishi kuondoka nchini humo na
kukabidhi madaraka.
Post a Comment