Mshindi wa Ubunge Dimani aahidi kuwa daraja
Mshindi
wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar Juma Ali
Juma ameahidi kuzibeba kero za wananchi wa jimbo hilo na kuwasilisha
serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa haraka
Ametoa
ahadi hiyo mara baada ya Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo, Fatma Gharib
Ali kumtangaza rasmi kuwa mshindi katika uchaguzi huo na kusema kuwa
kuwa Ubunge ni daraja la wananchi na serikali
Uchaguzi
huo mdogo umefanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo Hafidh Ali Tahir akiwa Bungeni Dodoma na umehusisha wagombea kutoka
vyama 11 vya siasa.
Juma Ali Juma amepata kura 4,860 na kumshinda mpinzani wake kutoka CUF, Abdulrazak Khatib Ramadhan aliyepata kura 1,234.
Katika
Uchaguzi huo wapiga kura walikuwa 6, 172 kati ya wapiga kura 9,275
waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura jimboni humo.
Katibu
wa Idara Maalum ya NEC, Itikadi na Uenezi Zanzibar amesema ushindi wa
mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi huo umekuwa mkubwa kuliko ule wa
uchaguzi wa mwaka 2015, ishara inayotoa matumaini ya kuwa wananchi wa
jimbo hilo wanaendelea kuiunga mkono CCM.
Post a Comment