Meli ya Kisasa ya Azam Yatia Nanga Bandari ya Tanga kwa Mara ya Kwanza
TANGA:
Meli mpya na ya kisasa iitwayo AZAM SEALINK 2 aina ya RORO yenye uwezo
wa kubeba abiria wapatao 1650, mizigo uzito wa tani 717 sambamba na
magari 150 imetia nanga kwa mara ya kwanza katika Bandari ya Tanga leo,
Januari 30, 2017.
Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake na kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo ikiwemo magari kutoka Pemba kwenda Unguja hadi Tanga mara moja kwa wiki.
Meli hiyo inatarajiwa kupunguza adha
ya uisafiri katika bandari hiyo sambamba na kurahisisha usafirishaji wa
mizigo, magari pamoja na abiria kupitia Bandari ya Tanga.
Muonekano wa meli hiyo kwa nje.
Post a Comment