Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humprey Polepole atangaza neema kwa Wanafunzi waliokosa mikopo
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humprey Polepole
amewatangazia neema wanafunzi wa elimu ya juu waliokosa mikopo,
akiwataka wamtafute ili awaoneshe cha kufanya
Polepole ambaye alikuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV
aliuzwa na baadhi ya watu kuhusu tatizo lililopo la mikopo ya elimu ya
juu, ambapo aliwajibu kuwa serikali imekwishatoa maelekezo kwamba
haiwezi kumkopesha kila mtu na kwamba inatoa mikopo kwa vigezo
vilivyowekwa.
Kuhusu
watu wasioweza kujigharamia elimu hiyo na wamekosa mikopo, amewashauri
kuahirisha masomo yao, ili wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata pesa
na ndani ya mwaka mmoja ana uhakika watakuwa wamepata pesa
zinazohitajika na kuendelea na masomo yao.
Polepole
alitaja baadhi ya shughuli ambazo angewashauri wazifanye kuwa ni pamoja
na kilimo huku akitolea mfano baadhi ya watu aliowashauri wajiingize
kwenye kilimo cha matikiti na wakaufanyia kazi ushauri huo, ambapo baada
ya muda wameona matunda yake.
"Waliokosa mikopo vyuo vikuu wanitafute, nitawaonesha cha kufanya, na wawe tayari kuahirisha masomo mwaka mmoja"
Akizungumzia
uamuzi wa serikali kusimamisha ajira, Polepole amesema serikali haiwezi
kuendelea kuajiri wakati inafanya kazi ya kuondoa wafanyakazi hewa
ambao wanalitia hasara taifa na kuwataka watanzania waendelee kuwa
watulivu na kumuunga mkono Rais Magufuli, ili amalize mchwa wote
serikali na kisha ajira zitatoka.
"Nawaambia vijana wakati unasubiri ajira usibweteke kwani mtu anayebweteka akipata kazi ataharibu kazi yetu"
Kuhusu
serikali kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati pekee,
Polepole amesema uamuzi huo ni sahihi kwa kuwa taifa lina uhaba mkubwa
wa walimu wa Sayansi na Hisabati kuliko walimu wa masomo ya sanaa.
"Tunao utimilifu wa walimu wa sanaa, tunao upungufu wa walimu wa Sayansi"
Post a Comment