Jeshi la Senegal Laingia Gambia Kukabiliana na Rais Jammeh Aliyegoma Kuondoka Madarakani
GAMBIA: Vikosi vya majeshi kutoka nchini Senegal vimethibitisha kuingia katika ardhi ya Gambia katika muda ambao rais mpya Adama Barrow alipokuwa akiapishwa kwa lengo la kumuondoa madarakani Rais Jammeh aliyeng’ang’ania uatawala baada ya kushindwa uchaguzi.
Msemaji wa Jeshi la Senegal Kanali Abdou
Ndiaye amethibitisha kwamba vikosi hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua
kuelekea katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Banjul na kusema kwamba vikosi
hivyo mpaka sasa havijakabiliana na ukinzani wa aina yoyote ingawa
viliweka bayana kwamba vilikuwa vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.Picha zote na maktaba.
Mapema Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa inasemekana kwa siri limekuwa likiunga mkono juhudi za vikosi
vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais Barrow anachukua madaraka kutoka kwa
rais aliyemaliza muda wake Yahya Jammeh. Rais huyo wa zamani wa Gambia,
awali aligoma kuachilia madaraka.
Rais wa sasa Adama Barrow ameapishwa leo
katika nchini jirani kwenye ubalozi wa Gambia ulioko mjini Dakar nchini
Senegal na kufuatiwa na shamra shamra ubalozini hapo.
Mpaka sasa haijafahamika wazi lini rais
mpya wa Gambia ataweza kurejea nchini mwake na kuchukua hatamu za
uongozi kwa mara ya kwanza akiwa rais.
Post a Comment