HII NDIYO KAULI YA TFF BAADA YA SAANYA WALIYEMFUNGIA KUPEWA SHAVU NA CAF
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHeWxXWDOF9_w5irfy4vBq84BNZo0KmaHTlAyB4IkY8Lqk6w3bCiDqDsLUF9zo6-x9oQjOVojVfetfovPJWf4APIn3T-4BvY8jynQ4xbIpmtWTuov9g2dnjvqGA2yrBfPq4wVFqdZ9ho8/s640/Saanya+Martin+%25289%2529.jpg)
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limetoa ufafanuzi wake kuhusiana na Shirikisho
la Soka la Afrika (Caf) kumteua mwamuzi Martin Saanya kuchezesha mechi
za kimataifa wakati amefungiwa na TFF kujihusisha na soka.
Hivi
karibuni Caf ilimtangaza Saanya kuwa mmoja kati ya waamuzi
watakaochezesha mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika namba 18
utakaozikutanisha Vital’O ya Burundi na Mountana ya Sudan.
Akizungumza
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema: “Saanya ni mwamuzi wa Fifa
(Shirikisho la Soka la Kimataifa), hivyo kitendo cha kufungiwa
kuchezesha mechi za Ligi Kuu Bara hakiwezi kumzuia kuchezesha mechi za
kimataifa ambazo zinasimamiwa wa Caf pamoja na Fifa.
“Baada
ya kuvurunda katika mechi za ligi kuu tulizompatia achezeshe, tukaona
hatufai, hivyo tukaamua kumweka pembeni lakini Caf wao wameona anafaa
kwa sababu alifanya mtihani wao pamoja na ule wa Fifa akafanya vizuri,
hivyo wana haki ya kumtumia.”
TFF
ilimfungia Saanya pamoja na aliyekuwa msaidizi wake katika mchezo wa
Ligi Kuu Bara, Samuel Mpenzu katika mchezo uliozikutanisha Simba na
Yanga Oktoba Mosi, mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam baada ya kudaiwa kuvurunda mechi hiyo kwa kutoa maamuzi yenye
utata likiwemo tukio la kumwonyesha kadi nyekundu Jonas Mkude wa Simba.
Pia
Saanya alishindwa kutoa maamuzi sahihi juu ya bao la Yanga ambalo
lilifungwa na Amissi Tambwe ambaye kabla ya kufunga alidaiwa kuushika
mpira.
Post a Comment