Dada wa Diamond Platnumz afunguka kuwa huwa hatongozwaji bali huwa anatongoza..!!!
MWANAMUZIKI ambaye ni memba wa Kundi la WCB, Mwanaisha Abdul ‘Queen
Darleen’ aliye pia dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ametoa
kali ya mwaka baada ya kufunguka kuwa katika mapenzi kitu ambacho
hakipendi ni kutongozwa na mwanaume hivyo huwa anapenda kutongoza.
Akistorisha na Mikito Nusunusu Darleen,
alisema kitendo cha yeye kumtongoza mwanaume anaamini kwamba anakuwa
amempenda kutoka ndani ya moyo wake lakini akitongozwa wakati mwingine
wanaume wanakuwa ni waongo hawana nia ya dhati.
“Katika maisha yangu yote huwa
sipendi kutongozwa napenda nitongoze kwa sababu naamini nikifanya hivyo
nakuwa nimempenda mwanaume kweli kwani watongozaji wengi ni waongo na
ninajijua kabisa kwamba sina bahati kwenye mapenzi,” alisema.
Post a Comment