BREAKING NEWS: KAHEMELE AACHIA NGAZI SIMBA
Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele ameachia ngazi.
Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa Kahemele zinaeleza aliandika barua na kamati ya utendaji ya Simba, imepitisha hilo.
Upande mwingine wa taarifa, umeeleza Kahemele anarejea na kujiunga na Azam TV ambako alikuwa akifanya kazi kabla.
“Kweli anaondoka, leo kamati ya utendaji ya Simba imekubaliana naye,” kilieleza chanzo.
Juhudi za kuwapata viongozi wa Simba walizungumzie hilo, zinaendelea.
Post a Comment