SAKATA LA POLISI KUMDAKA MSUVA PALE TAIFA HUKU MASHABIKI 'WAKIMRUKIA' CANNAVARO LILIKUWA HIVI

Sare
ya bao 1-1 iliyopata Yanga dhidi ya African Lyon, jana ilikuwa chungu
na kusababisha hali ya sintofahamu baada ya baadhi ya mashabiki wa Yanga
kukasirishwa na matokeo hayo na kuzua varangati kiasi kwa wachezaji wa
timu hiyo.
Matokeo
hayo ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ambayo yanaifanya Yanga iendelee
kubaki nafasi ya pili katika msimamo wa hiyo kwa kufikisha pointi 37
nyuma ya Simba yenye pointi 38, yaliwakasirisha baaadhi ya mashabiki
walioamini kuwa wachezaji wao walifanya uzembe na ndiyo maana
waliambulia pointi moja katika mchezo huo.
Nahodha
wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Simon Msuva katika nyakati
tofauti walijikuta katika mazingira magumu baada ya mchezo huo
uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
MASHABIKI WAMVAA CANNAVARO
Baada
ya mchezo huo mashabiki kadhaa wa Yanga wakionekana kuwa na hasira,
walikuwa wakilalamika kuwa kitendo cha wachezaji kucheleweshewa mshahara
wao wanaodai kimesababisha wacheze chini ya kiwango.
Kutokana
na mashabiki hao kuonyesha hasira, ilibidi basi linalowabeba wachezaji
wa Yanga liingie ndani ya uwanja kwa ajili ya kuwachukua lakini wengine
wachache walielekea kwenye magari yao binafsi.
Wakati
Cannavaro akitoka, ghafla alivamiwa na mashabiki waliokuwa wakimlaumu
kwa matokeo hayo, baada ya muda uvumilivu ukamshinda na kujikuta
akiwajibu kwa lugha kali, hali iliyosababisha mvutano na kutaka kupigana
lakini daktari wa zamani wa Yanga, Juma Sufiani aliingilia kati na
kumuondoa kisha kumpeleka kwenye gari lake.
Mashabiki
hao walibaki wakitoa lugha kali huku wakilalamika wakati basi la
wachezaji likitoka mlango wa nyuma na kuondoka huku mashabiki wengi
wakiendelea kulisubiri upande wa mbele.
WACHEZAJI WATOA KAULI NZITO
Mchezaji
mmoja wa Yanga (jina kapuni) akionekana kupandwa na hasira baada ya
mchezo huo aliwajibu hovyo mashabiki wa timu yake waliokuwa
wakilalamikia matokeo hayo kwa kusema: “Tumefanya kusudi na bado.”
Mwingine
ambaye alianza katika kikosi cha kwanza cha jana, alisema bado
hawajalipwa madai yao yaliyosababisha wagomee mazoezi wiki hii licha ya
kuahidiwa kutimiziwa haki yao hiyo jana asubuhi.
MSUVA AKAMATWA
Wakati
akitoka uwanjani hapo akiwa ndani ya gari lake aina ya Toyota Altezza,
Msuva alisimama pembeni kidogo ya barabara, ghafla askari wa usalama
barabarani walimfuata na kumwambia amesimama sehemu ambayo hatakiwi
kuegesha gari.
Msuva
akajitetea kuwa alikuwa akimsubiri mchezaji mwenzake, Ramadhani Kessy
ambaye kweli alifika baada ya dakika kadhaa lakini askari hao
hawakumuelewa, badala yake wakamtaka aende kituoni au alipe faini ya Sh
30,000.
Kuona
hivyo, mashabiki wakaongezeka kwa wingi eneo hilo la tukio na
kuwabembeleza askari hao lakini msimamo ulikuwa ni uleule, ndiyo
wakalazimika kuchanga kiasi hicho cha fedha na kumlipia Msuva ndipo
akaruhusiwa kuondoka huku akiwashukuru mashabiki hao.
MCHEZO ULIVYOKUWA
Baada
ya kupata ushindi katika mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu wa mabao
3-0, kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina ameshindwa kuendeleza kasi
yake ya ushindi.
Lyon
ilianza kufunga kupitia kwa Venance Ludovick katika dakika ya 59, Yanga
ilisawazisha katika dakika ya 74 mfungaji akiwa ni Amissi Tambwe
aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Juma Abdul.
Tambwe atoa bao kwa mtoto
Akizungumza
na gazeti hili, Tambwe aliyeshangilia kwa staili ya kunyonya kidole
baada ya kufunga, alisema: “Bao nililofunga ni zawadi maalum kwa
mwanangu (Amiyan) ambaye nimempata wiki hii baada ya mke wangu (Raiyan)
kujifungua.”
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment