Polepole Ateuliwa Kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Kuchukua Nafasi ya Nape Nnauye
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey PolePole ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu
Itikadi na Uenezi kuchukua nafasi ya Nape Nnauye
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimemteua Ndg @hpolepole kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) December 13, 2016 nt-family: "arial" , "helvetica" , sans-serif;">
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia ukurasa wake wa
Twitter zinaeleza kuwa kikao chaHalmashauri Kuu ya Taifa kimemteua
Polepole kushika wadhifa huo.
Kikao
cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kimefanyika leo ambapo miongoni mwa
mambo mengi yatakayojadiliwa ni pamoja na tathmini ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015.

Post a Comment