MBAO FC, KAGERA SUGAR KUCHEZA MECHI YA KUMCHANGIA STRAIKA ALIYEFIA UWANJANI
![]() |
| ISMAIL WAKATI AKIWA NCHINI MAREKANI |
LEO Jumamosi Desemba 10, 2016 kutakuwa na mchezo maalumu wa kirafiki
utakaozikutanisha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara Mbao FC
na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo
huo utakaoanza saa 10.00 jioni utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kutoa
heshima kwa marehemu Ismail Khalfan - mchezaji wa timu ya vijana Mbao
aliyefariki dunia Desemba 4, mwaka huu wakati akiiitumikia timu yake ya
vijana kwenye mchezo wa Ligi ya Vijana ya TFF U20 dhidi ya Mwadui,
uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Mbali
ya kutoa heshima kwa marehemu Khalfan, pia waratibu wa mchezo huo
wakiwamo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Mwanza na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA),
wamepanga mapato yake yote ni kutoa rambirambi kwa familia ya Khalfan
iliyopoteza ndugu yao mchezoni.
TFF,
KRFA, MZFA na wadau wengine wangali wakitoa pole kwa familia kwa msiba
kwa familia kwa msiba wa Ismail Khalfan ambaye pia ameombolezwa na
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Rais wa
CAF, Issa Hayatou.
Kadhalika,
mchezo huo utatumika kama kuzipima nguvu timu hizo baada ya mapumziko
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) hivyo wadau wote wa michezo wameombwa
kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuchagia rambirambi ya familia hiyo
ambayo kwa pamoja na wanafamilia ya soka walipoteza hazina nyingine
muhimu kwenye mpira wa miguu.


Post a Comment