Kwa Mpango Huu, Azam FC Wanaiba Fedha Za Bakhresa
Selemani Matola
MIAKA 20 iliyopita tofauti na Simba na Yanga, kulikuwa na klabu kadhaa zilizoibuka na kutoa ushindani mkali kwenye soka la Tanzania lakini baada ya muda zilipoteza na wababe hao wawili ambao maskani yao ni Kariakoo jijini Dar es Salaam walibaki na kuendelea kutesa.
Ni jambo la kipekee kuwa na timu mbili kubwa ambazo zinaweza kuendelea kuwa kubwa miaka na miaka, kizazi na kizazi, lakini pamoja na hiyo tunatakiwa kukubali kuwa upinzani wa zamani na sasa una utofauti kutokana na changamoto kadhaa.
Ili ligi iwe bora ni vema hata timu nyingine katika ligi nazo ziwe bora kuliko kuzitegemea Simba na Yanga. Tazama England kwa sasa ligi kuu yao zamani ilikuwa na timu nne kubwa lakini leo hii unaweza kusema Premier League ina timu sita au saba bora na zote zinaweza kuwania ubingwa.
Enzi zetu wakati nacheza soka na kabla yetu ilikuwa unatakiwa kuonyesha uwezo wa juu ili usajiliwe Simba au Yanga kwa kuwa ndiyo zilikuwa timu kubwa na ambazo angalau unaweza kupata maslahi mazuri kiasi.
Ujio wa Azam FC, katika Ligi Kuu Bara nilitambua inaweza kuwa klabu yenye kutoa ushindani kutokana na mipango na jinsi ambavyo wamiliki wake walikuwa wakionyesha nia ya kuiboresha klabu hiyo.
Azam ambayo ilianzishwa mwaka 2007 iliendelea kuwa na mipango mizuri mpaka ikafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ndani ya miaka michache tu, hayo yalikuwa maajabu na yalionyesha wazi kuwa soka sasa ni uwekezaji, bila kufanya hivyo ni rahisi kupoteza mwelekeo na ni ngumu kupata mafanikio.
Simba na Yanga ni klabu kubwa lakini zimeshindwa kupata mafanikio kwa kuwa kuna mambo mengi yanafanywa kienyeji na hakuna uwekezaji wa kueleweka, klabu hizo zinategemea nguvu za watu binafsi kujiendesha, wanapokosekana watu wa aina hiyo huwa ni kawaida kuona kukiwa na kupoteza dira.
Ukongwe wa timu hizo umechangia kwa kiwango kikubwa kupata nafasi ya kuwakilisha taifa kimataifa lakini zimeshindwa kufanya vizuri huko kwa kuwa asilimia kubwa zimekuwa zikikutana na watu waliojipanga vizuri na wenye uwekezaji tofauti na wao.
Unapozungumzia uwekezaji naweza kusema kwa soka la Tanzania, Azam ndiyo klabu yenye miundo mbinu bora kuliko nyingine zote, hapa nazungumzia kuanzia maslahi, huduma nzuri kwa wachezaji, viwanja bora vya mechi na mazoezi, mazingira mazuri ya kucheza, huduma za afya na mengine mengi.
Azam ndiyo ilikuwa moja ya klabu za kwanza kuwa na mipango bora ya kukuza soka la vijana hata kabla ya Simba kipindi kile mimi nilipokuwa kocha wa vijana wa Simba.
Nilikuwa nikifundisha Simba lakini niliamini Azam ndiyo watakaotengeneza wachezaji bora kutokana na mazingira ya klabu yao na jinsi walivyokuwa wakijiendesha, lakini imekuwa kinyume kabisa.
Tazama zao la wachezaji wa Simba na wale wa Azam wa kipindi kile, Azam imeshindwa kufikia malengo kwa kiwango cha juu, zaidi ya Farid Mussa na wengine wachache, bado klabu hiyo imeshindwa kufanikisha kile ambacho kilikuwa kikiwekezwa na mabosi wa timu hiyo.
Baada ya mafanikio ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa timu kubwa ilionekana kama klabu hiyo imepoteza mwelekeo na kufumuliwa kila mara hali ambayo ilionyesha kama vile viongozi hawajui wanachotaka.
Vijana wa Simba kina Said Ndemla, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Ramadhani Singano na wengine wote walikuwa kizazi kimoja na wale wa Azam, lakini linganisha kilichozalishwa katika pande hizo mbili, utapata jibu.
Mfano hivi juzi, Simba ambayo ina wachezaji wa kuungaunga wa timu ya vijana ndiyo ambao wametwaa kombe wakati Azam kuna uwekezaji mkubwa lakini ilikwama.
Azam inasajili wachezaji wengi kwa mamilioni ya fedha, wengine wanatoka wengine wanaingia lakini bado mafanikio hayaonekani na ndani ya muda mfupi unaona wanapishana kila dirisha la usajili kiasi kwamba inaonekana kama bado hawaelewi nini wanachotaka.
Tazama msimamo wa ligi kuu ulivyo sasa, Azam ambayo pia ina makocha kutoka Hispania ambao naamini wanalipwa vizuri, inashika nafasi ya tatu huku ikizidiwa pointi 12 na Simba inayoshika usukani.
Wanaweza kusema wanatengeneza timu lakini pamoja na hivyo nahisi wanatakiwa kutuambia kuna tatizo gani nyuma ya pazia, tofauti na hapo watakuwa hawazitendei haki fedha za mmiliki wa Kiwanda cha Azam, Said Bakhresa ambaye kiwanda chake kinaimiliki hiyo timu.
Kiasi kingi cha fedha kinachotolewa klabuni hapo huku matunda yakiwa ni madogo, binafsi naona ni kama wanaiba fedha hizo kwa kuwa kinachotoka na kinachorudi ili kiwe faida havifanani, labda kama wanafidia faida inayopatikana kwenye matangazo yao ya bidhaa wanazotangaza katika jezi.

Post a Comment