Wanasayansi Udsm Wafurahia Kuhitimu
WANACHUO wa kitengo
cha sayansi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mapema leo wameonekana wakifurahia
kuhitimu masomo yao ambapo kamera yetu imewashuhudia wakipiga picha mbalimbali
chuoni hapo kabla ya kuelekea kwenye Ukumbi wa Mlimani City, kulipofanyika
sherehe za mahafari ya 46 ya chuo hicho.
Mmoja wa wahitimu
hao aliyejitambulisha kwa jina la Dauson Amos akizungumza na mtandao huu
alisema, anamshukuru Mungu kwa kuweza kuhitimu masomo yake hayo ya sayansi.
Mbali na mahafari
hayo kwa wanasayansi, mahafari mengine kwa ajili ya kozi nyingine chuoni hapo
yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Post a Comment