WAKATI BUSUNGU ANAIWAZA YANGA, KLABU NYINGINE ZAMUONA LULU, ZATAKA KUMNASA
Pamoja
na yeye kuahidi kurejea Yanga kwa kasi, klabu nne za Ligi Kuu Bara
zikiwemo Stand United, Tanzania Prisons, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar
zimejikuta zikigongana katika Klabu ya Yanga kumuwania mshambuliaji
Malimi Busungu kwa ajili ya kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili
linaloendelea hivi sasa.
Busugu
aliingia mgogoro na benchi la ufundi la timu hiyo na kuamua kutimka
kikosini hapo kutokana na kutopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha
kwanza.
Meneja
wa Busungu, Yahya Tostao, amesema hadi sasa Yanga haijawapa taarifa
yoyote juu ya kuendelea ama kuachana na mchezaji huyo huku wakiwa
wamepokea barua kutoka katika timu nne za ligi kuu.
“Bado
Yanga haijatupa taarifa yoyote juu ya kuendelea ama kutoendelea na
Busungu, hivyo tunawasubiri wao iwapo watahitaji kumtoa kwa mkopo basi
tutazungumza nao kuweza kujua maslahi ya mchezaji,” alisema Tostao.
Post a Comment