SUALA LA KESSY LAINGIA KWENYE DANADANA, LAHAMISHIWA KAMATI NYINGINE ITOE MAAMUZI!
Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilikutana jana Jumapili Novemba
27, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bodi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kupitia mashauri manane.
Shauri la 1. Klabu ya Simba dhidi ya Young Africans na mchezaji Hassan Hamis Ramadhani Kessy
Shauri
hili sasa limerudi rasmi kwenye meza ya Kamati ya Katiba, Sheria na
Hadhi za Wachezaji. Kamati iliyoketi chini ya Makamu Mwenyekiti,
Mwanasheria Raymond Wawa imekubali shauri hilo kurejea kwenye Kamati
yake na imeahidi kutoa maamuzi ndani ya wiki hii.
Shauri la 2. Malalamiko ya Ayoub Nyenzi na wenzake
Shauri
hili pia limepangwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki hii. Uongozi wa Young
Africans, umeagizwa kuleta nyaraka/kesi inayodai kuwa viongozi hao
waliofukuzwa uanachama na Mkutano Mkuu wa dharura ama walishiriki au
walifungua shauri mahakamani.
Uongozi
wa Young Africans, chini ya Kaimu Katibu Mkuu Baraka Deusdedit
ulikubali kuwasilisha nyaraka hizo kabla ya kikao kijacho
kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Wenzake na Nyenzi ni
Hashim Abdallah na Salum Mkemi.
Shauri la 3. Klabu ya Simba na Kocha Amatre Richard
Kamati
ilijikita kwenye hukumu yake na kuitaka Sekretarieti ya TFF kuandikia
Simba kuhusu msimamo wa hukumu iliyotolewa kwa Simba kumlipa kocha huyo.
Shauri la 4. Malalamiko ya Young Africans dhidi ya Kagera Sugar.
Wahusika
kwenye shauri hili, wameamuliwa kwenda Dar es Salaam mbele ya kikao
kitakachoitishwa mwishoni mwa wiki ili kujieleza. Wahusika hao ni Young
Africans waliowasilisha malalamiko, Panone FC ya Kilimanjaro, Kagera
Sugar pamoja na mchezaji husika ili hatua stahiki zichukuliwe mara baada
ya kuwasikiliza.
Post a Comment