MSANII WILDAD KUTOKA THE INDUSTRY KAACHIA WIMBO MPYA MKITONI
Lebo ya The Industry iliyo chini ya umiliki wa kundi la Navykenzo yaachia ngoma nyingine ya msanii wao Wildad iitwayo "Get It On". Wimbo unapatikana Mkito na unaupata kwa kubofya link hii: http://bit.ly/GetITOn
Msanii
huyo wa RnB amekuja kuteka mioyo ya kina dada kwa muonekano na sauti
yake ambayo ni kivutio kikubwa katika kuimba kwake. Akizungumza mara
baada ya kuachia wimbo huo kwenye ofisi za Mkito, Masaki jijini Dar
Wildad amesema “Nimekuja kuleta ladha mpya ya RnB na kipaji changu ni
cha kipekee na lengo kubwa la ni kuvuka mipaka”.
Wildad
alijiunga na “The Industry” May mwaka huu wa 2016 na ngoma yake pamoja
na video vinaashiria kuwa ana matarajio makubwa ya kuifikisha RnB ya
Tanzania kwenye matawi ya juu.
Itazame hapa video yake ya “Get It On” kisha pakua Mkito hapa http://bit.ly/GetITOn

Post a Comment