Binti wa Chuo Kikuu cha Makumira Adaiwa Kubakwa Hadi Kufa Kisha Mwili Wake Kutupwa (Video ipo hapa)
Mapema jana zimesambaa Picha kwenye Mitandao ya kijamii ikimuonyesha Msichana anayefahamika kwa jina la JULIANA ISAWAFO Ambaye Amebakwa hadi Kufa na Kutupwa Nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).
Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho ambapo amethibitisha kwamba ni kweli Ameokotwa Msichana huyo Majira ya Saa tano asubuhi ya Leo akiwa Amekufa na mwili wake Kutelekezwa kwenye Shamba la Mpunga hatua chache nje ya Eneo la Chuo.

Anasema Msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la Chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa waalimu wa Sanaa Chuoni hapo.
Hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba Wanasikitika sana Kwa Tukio hilo kwani Msichana huyo alikuwa kama Dancer wa Matamasha ya Chuo cha Makumira.
Sikiliza Hapa chini:
Post a Comment