AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUZINDULIWA TANGA NOVEMBA 19, 2016
Azam
Sports Federation Cup (ASFC) itakayoshirikisha timu 86 msimu huu,
itaanza rasmi Novemba 19, 2016 kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika mkoani
Tanga.
Bingwa
wa Mkoa wa Tanga msimu 2015/2016, Muheza United itacheza Sifa Politan
ambayo ni Bingwa wa Temeke, Dar es Salaam – mchezo utakaofanyika Uwanja
wa Mkwakwani jijini humo.
Siku
hiyo kabla ya mchezo kutakuwa na shamrashamra kupamba michuano hiyo
zitakazoandaliwa na Wadhamini Azam Tv ambayo kwa msimu wa 2016/17
zimeongezwa timu 22 kutoka mabingwa wa mikoa-- Muheza na Sifa Politan ni
miongoni mwa timu hizo. Ongezeko hilo tofauti na msimu uliopita ambako
kulikuwa na timu 64.
Mwaka
huu kuna timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu zote
24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu zote 24 za Daraja la Pili (SDL)
na timu 22 za mabingwa wa mikoa. Mashindano hayo yatakuwa ni ya mtoani
na yataendeshwa kwa raundi tisa (9).
Raundi
ya Kwanza itashirikisha timu zote 22 za Mabingwa wa Mikoa katika
makundi manne ya timu sita na timu tano ambako timu mbili za juu
zitaingia raundi ya pili.
Raundi
ya Pili itashirikisha timu nane zilizofuzu za RCL katika raundi ya
kwanza na kujumlisha timu 24 za Daraja la Pili (SDL) kufanya jumla ya
timu zote kuwa 32 kwa hatua ya pili.
Raundi ya Tatu itashirikisha timu 16 zilizofuzu hatua ya pili kushindana ili kupata timu nane zitakazoingia hatua ya nne.
Raundi
ya Nne itashirikisha timu zote za Daraja la Kwanza (24) na kumulisha
timu nane (8) zilizoshinda Raundi ya Tatu (3) kufanya timu zote kuwa 32.
Raundi
ya Tano, itashirikisha timu 16 zilizofuzu Raundi ya Nne (4) na kumuisha
timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufanya
timu zote katika raundi hii kuwa 32.
Raundi ya Sita itashirikisha timu zote 16 zilizofuzu katika Raundi ya Tano na mzunguko huo utaitwa Hatua ya 16 Bora.
Raundi
ya Saba (7) itashirikisha timu nane zilizofuzu katika raundi ya sita na
mzunguko huo kutambuliwa kuwa Nane Bora au Hatua ya Robo fainali .
Raundi
ya Nane ambayo itashirikisha timu nne zilizofuzu Raundi ya Saba (Robo
Fainali) na mzunguko huo utatambuliwa kuwa ni Nusu Fainali.
Raundi
ya Tisa itashirikisha timu mbili zilizofuzu Raundi ya Nane na washindi
hao wa Nusu Fainali na kumpata Bingwa wa Azam Sport Federation Cup kwa
msimu wa 2016/2017.
Post a Comment