WALIONG'OA VITI TAIFA WAIPONZA SIMBA, SERIKALI KUTOA TAMKO MCHANA HUU
Serikali
inatoa tamko leo kuhusiana na uharibu wa viti zaidi ya 200 uliojitoteza
jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Simba, waling'oa viti na kuvirusha uwanjani baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga bao.
Kabla
ya kufunga, Tambwe aliunawa mpira. Jambo hilo lilionekana kuwaudhi
mashabiki hao ambao walianza kung'oa viti na kuvitupa uwanjani.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye atazungumza leo na waandishi wa habari.
Kwa hali ilivyo, kama si onyo lazima kutakuwa na adhabu ambayo hakika itakwenda kwa klabu ya Simba.

Post a Comment