SIMBA YAMCHARUKIA MWIGULU NCHEMBA, YAMKUMBUSHIA SAANYA NI ASKARI CHINI YA WIZARA YAKE NAYE ALIKWENDA MROGORO
| MWIGULU AKITETA JAMBO NA KOSA MSAIDIZI WA YANGA, JUMA MWAMBUSI |
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
2-10-2016
TAARIFA KWA UMMA
Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba
imesikitishwa sana na vitendo vilivyofanywa na baadhi ya washabiki
wetu,cha kuvunja sehemu ya viti vya Uwanja wa Taifa.kitendo kilichotokea
jana kwenye mchezo wetu wa Ligi kuu dhidi ya Timu ya Yanga.
Tungependa kuomba radhi kwa kadhia hii na klabu imekubali kulipia gharama za uharibifu huu.
Klabu itazungumza na wamiliki wa Uwanja huu kuona inalipaje gharama hizo.
Ni mategemeo yeti kuona jambo hili halitajikoze tena.
Lakini mbali na hayo klabu kesho
Jumatatu itawasilisha malalamiko rasmi juu ya uchezeshaji mbovu wa
waamuzi wa mchezo wa jana,hususan Mwamuzi wa kati Martin Sanya.
Sisi tunaamini vitendo viovu
vilivyofanywa na washabiki wetu vilisababishwa na uamuzi wa hovyo kupita
kiasi uliosababishwa na waamuzi hao.
Haieleweki ni kigezo gani mwamuzi huyo
alitumia kulikubali goli la 'mpira wa pete'la mshambuliaji wa Yanga
Amisi Tambwe na kulikataa goli halali la mshambuliaji wetu Ibrahim
Ajibu.
Pia tumeshangazwa na kitendo cha kumpa
kadi nyekundu nahodha wetu Jonas Mkude.ilhali kama nahodha alimfata
kwenda kumlalamikia kitendo chake cha kukubali goli la 'hovyo 'la
Tambwe.
Sote tumeona Sanya alijikwaa wakati anarudi nyuma na kuanguka,kisha kuanguka na kutoa kadi nyekundu kwa Mkude.
Tunajua safari hii Tff na bodi ya Ligi zitatoa adhabu kali kwa waamuzi hawa ili iwe fundisho kwa maamuzi ya hovyo ya aina hii.
Pia klabu italalamika kitendo cha vyumba
vyetu vya kubadilishia nguo(dressing room)kupuliziwa dawa zilizokuwa na
nia ya kuwaathiri wachezaji wetu kabla ya mechi kuanza.
Tutaziomba mamlaka zifanye uchunguzi wa
kina kubaini kitendo hiki kisicho cha kiungwana kinachosadikiwa kufanywa
na wapinzani wetu.
Tunajua dhamira yao ni kuwafanya
wachezaji wetu wachoke,lakini timu yetu ya Matabibu ilichukua hatua
sahihi za kuwafanya wachezaji wetu waweze kumaliza dakika Tisini za
mchezo kwa uwezo na weledi mkubwa.
Na mwisho klabu itoe malalamiko yake kwa Waziri wa mambo ya nchi,Mh Mwigulu Nchemba.
Waziri huyu bila shaka amesahau majukumu yake yake ya kazi na kugeuka kiongozi wa klabu ya Yanga.
Tunajua ni haki yake kuwa na mapenzi kwa
klabu aliyoichagua lakini vitendo vyake anavyovifanya vinaacha maswali
mengi kuliko majibu ukizingatia nafasi yake kama Waziri mwenye dhamana
ya kuongoza Wizara nyeti.
Itakumbukwa majuzi waziri huyu alifanya ziara Mkoani Morogoro kuzungumza na vikosi anavyoviongoza.
Na inajulikana pia Refarii wa mchezo wa jana Martin Sanya ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza mkoani Morogoro
Sote tulishuhudia Jana Mwigulu alishangilia goli la hovyo la mwajiriwa wake Sanya.
Pia waziri huyu alitoa kauli tata kuwa
angetamani siku moja klabu inayoshangilia wapinzani wa Yanga wakipigwa
mabomu ya machozi na Askari wa jeshi la Polisi.
Kauli hii aliitoa wakati wa sherehe za
kukabidhi zawadi kwa timu zilizoshinda msimu uliopita zilizoandaliwa na
wadhamini wa ligi.kampuni ya Vodacom.
Tunajiuliza yale mabomu ya jana pale Uwanja wa Taifa ndio utekelezaji wa maagizo ya boss Mwigulu?
Lakini pia matumizi ya rasilimali za
umma yakiwemo magari ya serikali ktk shughuli za mara kwa mara za klabu
ya Yanga napo kunaacha maswali mengi mno.
Wanasimba wanauliza kila Waziri
anayeshabikia Simba akiwepo Waziri Mkuu akifanya vitendo hivi kutakuwa
na utawala gani serikalini?
Imani yetu viongozi wakuu wa nchi
watamuonya mh Mwigulu,vingenevyo atatengeneza chuki baina ya washabiki
wa Simba dhidi ya serikali yao.
Mwigulu atambue klabu ya Simba ina mamilioni ya washabiki kama ilivyo klabu yake anayoishabikia.
Hatutarajii kuona 'mahaba'yake yasio na staha yanachochea jambo ovu kwa wanasimba na serikali yao wanayoiamini na kuipenda sana.
IMETOLEWA NA
KLABU YA SIMBA
SIMBA NGUVU MOJA
Post a Comment