Mpambano Wa Isha Mashauzi, Malkia Leyla Ulikuwa ‘Balaa’!
Baada ya Isha kuanza kukamua shabiki huyu alikunwa na hivyo kuvamia jukwaa kwenda kumtunza.
Mtangazaji wa Redio Times FM, Aisha Mbegu (kulia) akirusha sarafu ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kukamua kati ya Leyla na Isha. Kushoto ni mshereheshaji MC wa Jahazi, Mwasity Robert, na katikati ni mwakilishi wa Isha na Leyla.
Mtangazaji wa Redio Times FM, Aisha Mbegu (kulia) akirusha sarafu ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kukamua kati ya Leyla na Isha. Kushoto ni mshereheshaji MC wa Jahazi, Mwasity Robert, na katikati ni mwakilishi wa Isha na Leyla.
MASHABIKI wa
burudani, hususan muziki wa taarab,
usiku wa kuamkia jana walipata burudani ya aina yake wakati wakali wa muziki
huo, Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic kwa upande mmoja na Leyla
Rashid kwa upande mwingine akiwa na kundi
lake la Jahazi Modern Taarab, walipotoana kijasho kwenye onesho maalum la kutaka kujua nani
mkali kati yao.
Kabla ya
mpambano huo kulikuwa na ubishani mkali kwa mashabiki ambapo upande fulani
ulisema Isha ndiye mkali kuliko Leyla huku wengine wakisema “aaah, wapi bwana
Leyla ndiyo mkali zaidi; pale Isha haingii hata kwa nini”!
Hatma ya
ubishi huo ni mpambano uliowakutanisha wawili hao na kuwaacha mashabiki
wakijionea na kuamua wenyewe. Kabla ya wakali hao kupanda jukwaani
mshereheshaji wa shughuli hiyo, Aisha
Mbegu, wa Redio Times ilibidi arushe sarafu hewani ili kumpata mwanamuziki wa
kuanza kulivamia jukwaa maana walianza kutegeana. Baada ya sarafu kurushwa Isha
ndiye aliyeangukiwa na zali la kuanza kuonesha mavitu vyake jukwaani.
Post a Comment