KAMPUNI YA BIN SLUM YAENDELEA KUINUA MICHEZO, YAWAPIGA JEKI KANDANDA
Kampuni
ya uuzaji matairi nchini ya Bin Slum Tyres Ltd,imeendeleza utamaduni
wake wa kulidhamini tamasha la ‘Kandanda Day’,ambalo litafanyika Oktoba
15,mwaka huu katika uwanja wa Jakaya M Kikwete Park,Kidogo Chekundu.
Mratibu
wa tamasha hilo,Fatma Dahir,amesema kwamba wanaishukuru kampuni hiyo
inayoongoza kwa uuzaji matairi nchini kwa msaada wa fedha na vifaa kwa
ajili ya tamasha hilo linalobebwa na kauli mbiu Dawati na Mpira.
“Kwanza
kabisa tunapenda kuchukua fursa hii,kuishukuru sana kampuni ya Bin
Slum,kwa kutuamini na kuwa pamoja zaidi ya miaka miwili katika
kuhakikisha tamasha hili linaendelea kuboreka mwaka hadi mwaka,”alisema
na kuongeza
“Kwa
mwaka huu,kauli yetu mbiu ni Dawati na Mpira, ambayo lengo lake kuu ni
kuhakikisha sisi kama wanamichezo tunaunga mkono jitihada za Serikali
katika kuhakikisha shule zetu zina madawati ya kutosha,hivyo tunaamini
kwa ushirikiano wa wanamichezo wanaounda kundi la Kandanda kwenye
ukurasa wa facebook na wadau wengine,tunaweza kuchangia kitu kwa ajili
ya elimu yetu.”
Fatma
alisema, kwamba wanaamini udhamini wa fedha walioupata kutoka Bin
Slum,utakua chachu ya ulifanikisha tamasha la mwaka huu,kuwa bora zaidi
na kuweka historia kwa wanamichezo watakaoshiriki na shule itakayopata
msaada wa madawati.
Kwa
upande wa mwakilishi wa kampuni ya Binslum Tyres Ltd, Bwana Salim Said
Al Jabry, alisema kwamba wameamua kuendeleza utamaduni wao wa kuchangia
tamasha la kandanda pamoja na kuuunga mkono kampeni ya kuchangia
madawati nchini.
“Binslum
Tyres tunafuraha kubwa ya kuendelea kuwa sehemu ya udhamini,ikumbukwe
huu ni mwaka wa tatu kwa kampuni yetu kudhamini tamasha hili,ambalo
kwetu ni faraja kuona wadau wanakutana pamoja na kushiriki pia kuisaidia
jamii kupitia mchezo wa kandanda,”alisema Al Jabry na kuongeza:
“Kwa
hiyo mwaka huu mbali na kutoa jezi kwa timu mbili mwenyeji ya Team Dizo
Moja na Team Ismail,lakini pia tumetoa kiasi cha fedha kipatacho
milioni moja kwa ajili ya kuchangia mchango wetu wa madawati na shughuri
zingine za uendeshaji.”
Mwaka
huu tamasha hilo linatarajia kushirikisha timu mbalimbali za makampuni
ambazo zitacheza katika mfumo wa ligi,kabla ya mshindi kupatikana
katika mchezo wa fainali.
Mratibu wa Kandanda Day
Fatma Dahir
Post a Comment