BABA NGASSA AANZA KAZI BOMBA NA TOTO IKIICHAKAZA KAGERA 2-0 KWAO KAITABA, STAND YAKOMAA MBEYA
Stand
United jana jioni kwenye Uwanja wa Sokoine imekomaa na kutoka suluhu na
Mbeya City huku Toto African ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar
katika Ligi Kuu Bara.
Raha
ilikuwa kwa kocha mpya wa Toto, Khalfan Ngassa ambaye ni baba mzazi wa
kiungo mshambuliaji wa Fanja FC ya Oman, Mrisho Ngassa ambaye amepata
ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
| KHALFAN NGASSA |
Mabao ya Toto yalifungwa na Jamal Soud dakika ya 47 na Mohammed Soud dakika ya 80.
Kwenye
Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United ya Shinyanga imeonyesha
imebadilika msimu huu baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya
wenyeji wake Mbeya City.
Mbeya
City sasa imebaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 16 moja nyuma
ya vinara Simba. Mbeya City imepaa hadi nafasi ya nne na pointi 12.
Stand
United imeendeleza rekodi yake ya kutofungwa msimu huu kwani imecheza
mechi nane na imeshinda nne na kutoka sare nane. Mbeya City imecheza
mechi nane, imeshinda tatu, sare tatu na kufungwa mbili.
Post a Comment