WAHUNI WAIFUNGIA KAZI YANGA, WATEKA MTANDAO WAKE......
Klabu
ya Yanga imepata pigo baada ya hivi karibuni watu waliotajwa kuwa ni
matapeli, kuvamia na kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano wa klabu hiyo
ambao ulikuwa ukitumika kwa ajili ya kuwapasha habari wapenzi na
mashabiki wa timu hiyo.
Kwa
mujibu wa habari ambazo zimelifikia gazeti hili kutoka katika Kitengo
cha Habari na Mawasiliano cha klabu hiyo, watu hao wasiojulikana
walivamia akaunti rasmi za kijamii za klabu hiyo na kuharibu mfumo mzima
wa mawasiliano kwa kufuta kumbukumbu zote kwenye akaunti hizo.
Akaunti
za klabu hiyo zilizovamiwa na watu hao ni zile za mitandao ya kijamii
ya Fecebook na Instagram iliyokuwa ikijulikana kwa jina la @yangasc
ambazo zilikuwa zikitumika kwa ajili ya kuwafikishia taarifa wapenzi na
mashabiki wa timu hiyo.
“Imetusikitisha
sana kwani ni jambo la ajabu sana lakini tayari uchunguzi wa jambo hilo
umeshaanza na baadhi ya watu waliohusika na suala hilo tumeshawabaini
na inaonekana walifanya hivyo kwa chuki zao binafsi ambazo kimsingi
hazina nia nzuri na klabu yetu.
“Hata
hivyo, kila kitu kitakapokuwa sawa basi tutawataja watu hao ambao
baadhi yao waliwahi kuwa viongozi wa klabu yetu,” alisema kiongozi huyo
ambaye aliomba kutotajwa jina lake kutokana na sababu mbalimbali
alizozitoa ambazo gazeti hili liliziona kuwa ni za msingi.
Hata
hivyo, alipoulizwa juu ya suala hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka
Deusdedit, alikiri kutokea kwa jambo hilo na kudai kuwa jitihada za
kufungua akaunti mpya zimeshafanyika lakini pia wanaendelea na uchunguzi
wa kuwabaini wale wote waliofanya jambo hilo ili waweze kuwafikisha
katika mkono wa sheria.

Post a Comment