BAADA NGASSA KUVUNJA MKATABA SAUZ, HII NDIYO KAULI YA KOCHA WA YANGA...
| NGASSA |
Kocha
Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amempa ugumu aliyekuwa kiungo
mshambuliaji wa Free States ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa kurejea
kuichezea timu hiyo.
Hiyo,
ni siku moja tangu taarifa za kiungo huyo kusitisha mkataba wake wa
kuichezea Free States kwa makubaliano huku tetesi zikienea kuwa nyota
huyo atarejea kucheza Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu
Bara msimu huu.
Ngassa,
alisitisha mkataba wa kuendelea kukipiga Sauz kwa kile alichodai kuwa
timu hiyo haina malengo ya kutwaa ubingwa zaidi kushiriki kwenye ligi
kuu.
| PLUIJM |
Pluijm
alisema kwenye kikosi chake hahitaji kiungo mshambuliaji kwani tayari
anao wanne, tena vijana wenye uwezo mkubwa wa kuendana na kasi yake.
Pluijm
aliwataja viungo hao washambuliaji kuwa ni Mzambia, Obrey Chirwa, Juma
Mahadhi, Simon Msuva na Deus Kaseke ambao anaamini bado wana uwezo
mkubwa wa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu kutokana na umri wao.
Aliongeza
kuwa, haoni sababu ya kujaza viungo wengi washambuliaji kwenye kikosi
chake kutokana na kutokuwa na tatizo katika nafasi hiyo.
“Nimepata
taarifa za Ngassa kusitisha mkataba wake wa kuichezea Free States,
labda nikwambie tu, ni ngumu kwangu kusajili kiungo mshambuliaji katika
kikosi changu kwa hivi sasa, kwani tayari ninao wanne ambao ni vijana
wenye uwezo mkubwa wa kucheza.
“Wachezaji
wanaocheza nafasi hiyo (ya Ngassa) ni Chirwa, Mahadhi, Kaseke na Msuva,
wote ni wazuri. Tofauti na kasi yao ya kushambulia, pia wana uwezo wa
kufunga mabao, ni aina ya uchezaji aliyonayo Ngassa,” alisema Pluijm.
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment