Tekemeko la Ardhi Laikumba Kanda ya Ziwa, Nyumba Zaporomoka






Leo Septemba 10, 2016, tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa Ritcha 5.7 limeikumbuka mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa Kagera na Mwanza na kusababisha maafa makubwa ikiwemo nyumba za watu kubomolewa.
Maeneo yalioathirika zaidi kwa Tanzania ni, Bukoba, Nsuga (zote za Kagera) na Baadhi ya maeneo ya Mwanza.
Mbali na Mikoa hiyo ya Tanzania, pia tetemeko hilo limeikumba baadhi ya miji na majiji ya nchini Uganda ikiwemo KampalaMbarara iliyopo Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.
UPDATES:– Imearifiwa kuwa tetemeko hilo limerudia tena likiwa na mtikisiko mkubwa zaidi.
– Nyumba kadhaa zimebomolewa.
– Pia taarifa za vifo zimesikika.
Map of the testimonies received so far following the #earthquakeM5.7 in Lake Victoria Region, Tanzania 42 min ago
Map of the testimonies received so far following the #earthquakeM5.7 in Lake Victoria Region, Tanzania 42 min ago
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mjini Bukoba, imeeleza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kuokana na tetemeko hilo huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa vibaya na mpaka sasa wanaendelea kutibiwa hospitalini hapo.
Aidha baadhi ya majeruhi ambao hawakuumia sana walitibiwa na kuuhusiwa kuondoka hospitalini hapo kurejea majumbani kwao.
Picha za majeruhi wanaotibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bukoba
PICHA NA: ABDULLATIF YUNUS BAISY/GPL-BUKOBA
















Post a Comment