TATHMINI YAKINIFU KUELEKEA PAMBANO LA SIMBA NA YANGA KESHO
Na Ahmada Mwariko
Ukiwa
umesalia usiku mmoja tu kuelekea mpambano wa watani wa jadi katika
ligi kuu soka ya Tanzania Bara homa ya mpambano wa Simba na Yanga
inazidi kupamba moto huku kila upande ukitoa tambo kuwa wataibuka na
ushindi.
Bila
ubishi pamabano hili ni miongoni mwa Derby kubwa kabisa barani Afrika
linalovuta hisia za mashabiki wengi hata wale ambao si mashabiki wa
mpira lakini mwisho wa siku hutaka kujua matokeo ya mwisho ya mpambano
huo.
Safu hii inakuletea tathmini ya mpambano huo kuanzia safu ya ulinzi mpaka ushambuliaji.
NAFASI YA GOLIKIPA
Agban vs Mustapha
Katika
nafasi hii bila shaka Mustapha anaonekana kuwa na kiwango kizuri kuliko
Agban, mpaka sasa ameruhusu goli 1 tu tangia ligi ianze huku Agban
akiwa amesharuhusu magoli 2, japo hiyo haitoshi kumpa credit Mustapha au
Agban lakini makosa ya mara kwa mara yanayofanywa na Agban akiwa golini
kama ya kuwa na maamuzi yasiyo na uhakika wakati anakwenda kucheza
mpira, kutema mipira hovyo na sio mzuri kwenye kucheza krosi, endapo
udhaifu huu utajitokeza basi goli la Simba halitakuwa Salama.
NAFASI YA ULINZI
Hapa
tathmini inaonyesha Timu zote kuwa na ukuta bora lakini swala la uzoefu
linaweza kuleta tatizo kwa upande wa Simba kwani wana maingizo mapya
katika safu hiyo ambayo ni kwa mara ya kwanza wanacheza katika pambano
la kesho
Beki
ya Yanga inayoundwa kwa sasa na Bossou na Dante imekuwa imara na
haipitiki kirahisi na mpaka sasa ikiruhusu goli 1 tu, Mwinyi Haji
anaitendea vyema nafasi ya ke ya ulinzi wa kushoto huku Juma Abdul
akisimama vyema upande wa kulia na hawa ni miongoni mwa mabeki
wanaopandisha mashambulizi mara kwa mara.
Kwa
upande wa beki ya Simba muunganiko wa Mwanjale na Lufunga umekuwa
ukitumika zaidi na kocha Omong na umeonekana kutoa matunda mazuri japo
bado akipangwa Mwanjale na Juuko wanaweza pia kumaliza shughuli pale
katikati, mwajale ameonekana kuwa mpambanaji na anacheza kwa kujituma na
bila shaka kesho Donald Ngoma atakuwa chini ya Ulinzi wa Mzimbabwe
mwenzake.
SEHEMU YA KIUNGO
Nafasi
hii ni dhahiri kabisa Simba imeimeza Yanga kwa kuwa na mafundi wengi
kuliko wenzao wa Yanga. Simba wanachagizwa na viungo wengi vijana ambao
wanacheza kwa nguvu na wajanja zaidi ya wale wa Yanga ambao kwa kiasi
kikubwa wanamtegemea Kamusoko katika eneo hilo na endapo atazidiwa basi
ni dhahiri hali itakuwa mbaya kwa upande wa Yanga
Mpira
wa sasa unategemea sana safu ya kiungo kupandisha Timu na kutengeneza
nafasi za kufunga..Roation ya kikosi kwa Timu ya Simba kutaisaidia
kufanya vyema katika safu hii.
NAFASI YA USHAMBULIAJI
Yanga
wamekuwa na safu bora ya ushambuliaji ikiongozwa na Amis Tambwe na
Donald Ngoma huku ikichagizwa na Simon Msuva, wameskuwa ni wepesi
kufanya maamuzi kwenye lango la mpinzani na katika msimu uliopita Tambwe
na Ngoma walifanikiwa kuwafunga Simba katika mechi zote za ligi
walizokutana na tayari safu hii imeshafunga magoli 8.
Kwa
upande wa Simba ni kama hawatabiriki yani hujui nani wa kuchunga zaidi,
vijana kama Kichuya na Mnyate wamekuwa moto wa kuotea mbali wakati
unaendelea kumchunga Ajib na Mavugo vijana hawa wanawez kukudhuru wakati
wowote, wamekuwa na jitihada binafsi kutafuta magoli kwa hivyo safu ya
ushamuliaji wa Simba imejaa vipaji na haitabiriki nani atafunga
wachezaji wote wanne pale mbele wamekuwa hatari langoni mwa wapinzani
tayari safu hii imeshafunga magoi 12.
MAJUMUISHO
Ukomavu
na uzoefu wa wachezaji wa Yanga unaweza ukawa chachu ya ushindi katika
mechi ya Kesho lakini uchovu wa kucheza mechi nyingi bila kupumzika na
kutokuwa na Rotation ya Wachezaji katika kikosi cha Yanga inaweza
kuwagharimu na kupoteza mchezo huo.
Uchanga
wa kikosi cha simba na ugeni wa mpambano huu kunaweza kuigharimu timu
ya Simba na kupoteza mchezo lakini utimamu na utimilifu wa vipaji
walivyonavyo wachezaji wengi wa Simba, Rotation ya wachezaji
wanayoifanya katika mechi walizocheza inaweza kuwa chachu ya ushindi
katika mchezo huo.
Mwisho wa siku dakika 90'' ndio zitaamua nani ni nani kati ya Simba na Yanga

Post a Comment