CHANZO CHA NDEGE YA RONALDO KUPATA AJALI JIJINI BARCELONA CHABAINISHWA
Ndege ya mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo imepata ajali mjini Barcelona, Hispania.
Ndege
hiyo imepata ajali kwa kuteleza hadi kukwama kwenye majani na imeelezwa
sababu ya ajali hiyo ni kuvunjika kwa gia ambayo hutumika wakati wa
kutoa.
Ronaldo
hakuwa katika ndege hiyo wakati ikitua Barcelona na kupata ajali hiyo,
ila imeelezwa, tatizo hilo la gia ndiyo limekuwa chanzo.
Hakukuwa
na taarifa za majeruhi na ndege hiyo haikuumia zaidi ya kukwama kwenye
majani ingawa imeelezwa matengenezo yake, bado yatakuwa na gharama za
juu.




Post a Comment