LIVERPOOL YAITOA SHOO ARSENAL KWAO EMIRATES, YAICHAPA KWA MABAO 4-3
Liverpool
imeionyesha Arsenal si kitu kwake baada ya kuichapa mabao 4-3 licha ya
Arsenal kuwa nyumbani Emirates tena ikianza kufunga.
Arsenal
ilikuwa ya kwanza kufunga bao kupitia kwa Theo Walcott dakika ya 30,
ambaye muda mchache alikosa mkwaju wa penalti. Dakika ya 45, Coutinho
akasawazisha.
Adam Lallana akafunga dakika ya 49 huku Coutinho akiongeza bao la tatu dakika ya 56.
Arsenal
walianza kujipanga lakini kabla hawajakaa vizuri, Sadio Mane akafunga
bao la nne katika dakika ya 63 na kuwalazimu Arsenal kuongeza juhudi
hadi walipopata bao la pili katika dakika ya 64 kupitia Oxlade
Chamberlain.
Katika
mechi hiyo ya ufunguzi wa Ligi Kuu England, Arsenal iliongeza bao la
tatu katika dakika 75 kupitia Calum Chambers katika dakika ya 75 lakini
ikashindwa kupata bao la kusawazisha kwa dakika 25 zote za mwisho.
Post a Comment