JULIO AWA MAGUFULI WA KWENYE SOKA, AANZA NA KUMTUMBUA MSAIDIZI WAKE HABIB KONDO
Bosi
wa benchi la ufundi la Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ amesema msimu
wa 2016/17 ni mwendo wa Hapa Kazi Tu, hiyo ni kufuatia kumtimua kazini
aliyekuwa msaidizi wake, Habibu Kondo kwa kile alichosema anataka watu
wanaoendana na kasi yake.
Suala
la viongozi kutumbuliwa kutokana na uvivu au kutokuwa sahihi, limekuwa
maarufu sana kutokana na Rais John Magufuli kuanzia mfumo huo.
Julio
amesisitiza kauli yake ya kutaka ubingwa akisema ni msimu wa maajabu
kama Leicester City na katika kutaka kutekeleza hilo, ameamua kupitisha
panga kwenye benchi la ufundi baada ya kuanza na wachezaji kutoka 32 wa
msimu uliokwisha mpaka 23 atakaokuwa nao safari hii.
Kondo
amekiri kutokuwa na kikosi na kwamba viongozi wa Mwadui wamekuwa
wakimuahidi kumpa mkataba, lakini Julio mwenyewe amelifungukia Championi
Ijumaa, kuwa Kondo hana chake na tayari nafasi yake imezibwa na Khalid
Adam.
“Niliamua
tu kumuondoa na watu wengine ambao walikuwa hawaendani na sera yangu.
Nimedhamiria msimu huu ni wa Kazi Tu kama mheshimiwa rais (John
Magufuli) anavyosisitiza na mimi katika kutekeleza hilo nimeamua niwe na
benchi la ufundi la kazi tu na kikosi kidogo msimu huu.
“Nafasi
yake nimemkabidhi Khalid ambaye juzikati alipata leseni ya Daraja B na
ana weledi kwenye kitengo cha ukipa, hivyo atanisaidia sana kuwafundisha
makipa.
“Nimeamua
kuwa na ‘staff’ ndogo yenye ari, kasi ya kazi, siyo rundo la watu wa
kupiga porojo,” alifunguka beki huyo wa zamani wa Simba.
Aliwataja
miongoni mwa nyota aliowaongeza kuwa ni Salum Kanoni kutoka Kagera
Sugar, Nassor Masoud ‘Chollo’ (Stand United), Joseph Kimwaga (Azam)
Abdallah Seseme, Miraji Athumani (Toto Africans), Rashid Ismail (Simba),
William Lucian ‘Gallas’ (Ndanda) na kumrejesha Paul Nonga kutoka
Yanga.
Post a Comment