EXCLUSIVE...MANJI: HAKUNA ALIYEMFUNGIA MURO, HATUJUI LOLOTE KUHUSU HILO NA ANAENDELEA NA KAZI ZAKE KAMA KAWAIDA
Kama ulikuwa inaamini Jerry Muro amefungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ujue umekosea.
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji amesema hatambui lolote kuhusiana na kufungiwa
kwa Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo kongwe
zaidi nchini.
Akizungumza
na SALEHJEMBE, Manji amesema klabu hiyo inaendelea kumtambua Muro kama
mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano na anaendelea kufanya kazi
zake kama kawaida.
“Kama taarifa tumesikia kwenye magazeti na redio, kweli taasisi kama Yanga, msemaji wake anasimamishwa kwa njia hiyo.
“Hao
waliomsimamisha pia ni taasisi, vipi wafanye hivyo. Yanga tunawezaje
kuamini hilo? Muro bado yuko kazini na anaendelea na shughuli zake kama
kawaida,” alisema Manji.
Manji amesisitiza, kuwa kama ni kweli basi TFF inapaswa kutoa hukumu ya kumfungia Muro kama ambavyo wamekuwa wakisikia.
TFF kupitia kamati ya nidhamu ilitangaza kumfungia Muro mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kumpiga faini.
Lakini
imekuwa ikisita kutoa hukumu yake inayohusiana na Muro, jambo ambalo
linaifanya Yanga kuona kuna upotofu wa mambo na kukiukwa kwa usahihi.
Hukumu ya Muro imekuwa ni kitu cha uficho licha ya kamati hiyo chini ya TFF kumhukumu, jambo ambalo linaonekana ni kichekesho.
Post a Comment